HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 20, 2018

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILYA YA CHAMWINO

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Chamwino wakimshangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kuzungumza na watumishi hao, Oktoba 20, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga ordha ya watumishi ambao hawaishi kwenye kituo chao cha kazi cha Chamwino na badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa katika mazungumzo na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya wilaya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,  akisoma majina ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino  ambao hawaishi kwenye Kituo chao cha kazi cha Chamwino badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja  vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chamwino.

No comments:

Post a Comment

Pages