NA MWANDISHI WETU
UNAWEZA kusema walimu wameamua kufanya kweli na SportPesa
baada ya mwalimu, Noah Naumia wa Shule ya Sekondari ya Mkomazi (pichani), kukabidhiwa
bajaj mpya kutokana na kuwa mshindi wa droo ya 21.
Timu ya ushindi kutoka SportPesa imemkabidhi bajaj yake
mbele ya waalimu wenzake shuleni hapo, iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga.
“Nimefurahi kwa kuwa kile nilichokuwa nakitafuta baada ya
kubashiri na SportPesa kwa karibu mwaka mzima sasa nimekipata.
“Nategemea kuitumia bajaj hii iniongezee kipato na
naamini itanisaidia kujenga nyumba yangu ili kuepukana na usumbufu wa nyumba za
kupanga,” alisema.
Mke wa mshindi huyo, Mwalimu Esther Mpoki, hakuwa nyuma
kueleza furaha yake baada ya mumewe kushinda bajaj hiyo na kusema kuwa anaamini
itawasaidia kutatua matatizo mbalimbali katika familia yao ikiwemo kumsaidia
kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya vipodozi.
“Nimefurahia sana ushindi wa mume wangu, kwani bajaj hii
naamini itatusaidia kuanza kuweka akiba kwa ajili ya mtoto wetu Ivan, ili
akifikisha umri wa kuanza shule aweze kusoma shule nzuri kama nilivyokuwa
natamani iwe,” alisema mwalimu Esther.
Noah anakuwa mwalimu wa tatu kujishindia bajaj katika
promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa tangu ilipoanza, ambapo wateja wa
SportPesa hivi sasa mara baada ya kubashiri tu, namba zao huingizwa kwenye droo
na kuweza kujishindia bajaj mpya, simu za smartphone au jezi za ama Simba au
Yanga.
No comments:
Post a Comment