Na Munir Shemweta, WANMM Kilimanjaro
Serikali
imeziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha migogoro yote ya mipaka baina ya
vijiji na vijiji inaisha kabla ya desemba mwaka 2018.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipokutana na viongozi pamoja
na watendaji wa sekta ya rdhi katika halmashauri ya wilaya ya Same mkoani
Kilimanjaro mwishoni mwa ziara yake ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika
wilaya za Hai, Moshi na Same.
Alisema
halmashauri zote ni lazima zisimamie migogoro ya mipaka kati ya kijiji na kijiji
kwa kuwa ndiyo zenye mamlaka ya kusimamia pamoja na wajibu wa kurekebisha mipaka
pale unapotokea mgogoro wa pande mbili.
Kwa
mujibu wa Lukuvi, katika kushughulikia migogoro ya mipaka ya vitongoji, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) haina kumbukumbu za
majalada ya ardhi na wenye kumbukumbu hizo ni halmashauri husika hivyo
zinapaswa kuangalia, kugharamia na kusimamia kazi nzima ya kufanya marekebisho
ya mipaka pale unapotokea mgongano.
Alisema,
wakati serikali inaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani ni vyema
migogoro yote ya mipaka kati ya kijiji na kijiji pamoja na ile ya vitongoji
ikashughulikiwa mapema ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea wakati wa chaguzi
mbalimbali ukiwemo uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.
Katika
hatua nyingine, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleoa ya Makazi William Lukuvi
amezitaka halmashauri zote kuhakikisha idara za ardhi katika halmashauri zinafanya
kazi zake vizuri ikiwa ni pamoja kusimamia ukusanyaji kodi ya pango la ardhi.
Alibainisha
kuwa, kwa sasa Serikali haitamvumilia Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote
atakayeshindwa kuisimamia sekta ya ardhi na wakati huo kushindwa kufikia
malengo.
No comments:
Post a Comment