Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa I&M Bank, Ndabu Lilian
Swere, akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Benki hiyo
jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa promosheni ya 'Jidabo na
I&M Bank'. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji, Donald Mate
na kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo.
(Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa I&M Bank, Ndabu Lilian
Swere, akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Benki hiyo
jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa promosheni ya 'Jidabo na
I&M Bank'. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji, Donald Mate
na kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo.
(Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI
WETU
KATIKA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
Duniani, Benki ya I&M, imezindua promosheni ya ‘JIDABO na I&M Bank,’
ambayo mteja mpya anashiriki kwa kufungua Akaunti ya Akiba, Akaunti ya
Biashara, Akaunti ya Mshahara na Akaunti ya Mtoto.
Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani (Customer Service
Week), huadhimishwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, ambako
mwaka huu imeanza kuadhimishwa leo duniani kote.
Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa JIDABO
na I&M Bank, Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa Benki ya I&M,
Ndabu Lilian Swere, amesema wateja wapya wote watakaofungua akaunti hizo
kuanzia leo Oktoba Mosi hadi Desemba 31, wataingia katika promosheni hiyo.
“Kwa mteja ambaye tayari ana akaunti katika Benki ya
I&M, anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya kuanzia Sh. 200,000 kwa akaunti
ya biashara, na kuanzia Sh. 100,000 kwa akaunti nyinginezo, ili kuwa sehemu ya Promosheni
ya JIDABO na I&M Bank,” amesema Swere.
Amebainisha kuwa, kupitia JIDABO na I&M Bank,
mteja wa akaunti zilizotajwa watajiptia kiasi cha pesa mara mbili ya akiba zao
katika kipindi cha miezi mitatu, kupitia droo zitakazokuwa zinafanyika kila
mwaka.
“Washindi watano watakaopatikana kwenye droo hizo za
kila mwezi, watapata mara mbili ya akiba zao za mwezi, ambapo kiwango cha juu
kabisa kutolewa kwa mteja kitakuwa Sh. Milioni 5, ambaye atazdhiswa na kuwa Sh.
Milioni 10,” amesema Swere.
Ametoa wito kwa Watanzania wote, hususani wanaoishi
katika mikoa ya Dar es Salaaam, Mwanza, Arusha na (Moshi) Kilimanjaro,
kuchangamkia promosheni hiyo ya JIDABO na I&M Bank, ili kujiwekea nafasi za
kushinda na kujipatia pesa za kukamilisha malengo yao kuelekea mwisho wa mwaka.
No comments:
Post a Comment