Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Tigo, David Umoh (kulia) akizungumza na
waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa promosheni ya Data Kama Lote
inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti
watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya Tigo *147*00#, katika msimu
huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote. Kulia ni Mkuu wa Huduma za
Masoko wa Tigo, William Mpinga. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia)
akizungumza na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa promosheni ya
Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi
vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya Tigo
*147*00#, katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote. Kushoto
ni Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa Tigo, David Umoh.
Dar es Salaam, Oktoba 1, 2018 – Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni
murwa kwa wateja wote watakaonunua vifurushi vya intaneti kupitia menu
iliyoboreshwa ya *147*00#. Mteja
atapokea bonasi la uhakika papo kwa hapo lenye thamani hadi mara mbili ya
kifurushi cha intaneti atakachonunua katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018.
Akitangaza promosheni hiyo jijini Dar es
Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema, “Kuendana na
msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, promosheni hii ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa wateja
wote wa Tigo wanafurahia maisha ya kipekee ya kidigitali huku wakisambaza
matukio ya Tigo Fiesta 2018 mubashara kutoka sehemu yoyote ile ya nchi kupitia
mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa 4G+.”
Hali kadhalika, Tigo inatoa punguzo
kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia
Tigo Pesa Masterpass QR. Katika mikoa yote ya Tigo Fiesta 2018, wateja
wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua
namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda
namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia
shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha
Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila
wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila
moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki
wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI
kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua
Trivia.
Tigo ni mtandao unaojulikana kwa promosheni
kabambe na ubunifu wa kipekee unaoendana na mahitaji halisi ya soko, hivyo
kuifanya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa wateja wake zaidi.
Kwa hiyo tumejizatiti kuwapa wateja wetu
promosheni bora zaidi katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018. Tunawakaribisha
wateja wetu kufurahia ofa hizi murwa.
No comments:
Post a Comment