Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga akishukuru baaada ya kupokea shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya
ya Ilala Jijini Dar es Salaam
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam akishukuru kwa msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam
Katibu
wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw.
Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif
Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu
kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku
wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa
Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto)
No comments:
Post a Comment