Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kushoto) leo akiteta
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe
kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la
abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (aliyenyoosha mkono ukutani),
wakati akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati) na Mkurugenzi wa Kiwanja
cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha kwenye
ukumbi wa mikutano wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII).
Mafundi (kulia juu ya mashine)
wakiwa wanaendelea na ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere, wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Bw.Geoffrey Mwambe pamoja na msafara wao, leo
walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) anayesimamia mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la
abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII),
akielekeza jambo wakati wa ziara ya Wakurugenzi kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (wapili kushoto) na wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia) leo walipofanya ziara ya
kuangalia maendeleo ya mradi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (alinyoosha
mikono) leo akijaribu kueleza kwa vitendo katika ziara yake aliyoambatana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela (watatu kushoto) walipotembelea ujenzi wa mradi unaoendelea wa Jengo
la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, tayari
ujenzi umefikia asilimia 82.
No comments:
Post a Comment