Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma
salamu za rambirambi kwa familia ya mtangazaji wa zamani wa michezo
Ahmed Jongo (pichani), aliyefariki leo hospitali ya Temeke.
Kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa wafiwa,familia,ndugu,jamaa na marafiki kwa msiba huo.
“Nimepokea
kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Ahmed Jongo,kwa niaba ya TFF
natoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki,hakika tutamkumbuka kwa umahiri
wake wa kutangaza mpira wa miguu”.
Rais
wa TFF Ndugu Karia amesema Jongo enzi za uhai wake alipokuwa Radio
Tanzania Dar es Salaam RTD alikuwa chachu ya Watanzania wengi kufuatilia
mpira wa miguu kutokana na umahiri wake wa kutangaza mpira kupitia
matangazo ya moja kwa moja kwenye Radio.
Amesema
aina ya utangazaji wa mpira wa Jongo ulishawishi wengi kufuatilia mpira
wa miguu na kuhudhuria kutazama mechi mbalimbali.
Mungu ailaze roho ya marehemu Ahmed Jongo mahala pema pepino,Amen.
No comments:
Post a Comment