WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa kwenda
wilayani Kyerwa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji na
endapo atabaini ubadhilifu achukue hatua kwa watakaohusika.
Ametoa
kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 7, 2018) baada ya kukagua kiwanda cha
kukoboa kahawa cha Nkwenda wilaya Kyerwa katika siku ya pili ya ziara
yake ya kikazi mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana
na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
“Waziri
wa Maji na Umwagiliaji atakuja hapa kukakagua miradi yote ya maji
inayotekelezwa katika wilaya hii na pale atakapobaini ubadhilifu achukue
hatua.” Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka
kwa viongozi na mananchi wa wilaya hiyo baada ya kutoridhishwa na ujenzi
wa miradi ya maji.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo na wilaya ya Kyerwa ili kuwawezesha wananchi hasa wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo kuliko kutafuta maji.
Waziri Mkuu amesemaSerikali
kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo
kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata
huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka
kwenye makazi yao. Amewataka wananchi nao kutunza vyanzo vya maji ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
Amesema
nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma zote
muhimu, hivyo amewataka waendelee kuwa na imani na Serikali yao ambayo
imedhamiria kuwaboreshea maendeleo katika sekta za afya, maji, elimu ,
miundombinu na kilimo.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa mkoa wa Kagera kuwahamasisha
wananchi wake kujinga na Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF), ambao utawapa
fursa ya kupatiwa huduma za matibabu wao na familia zao kwa mwaka mzima
bure.
Awali,
Mbunge wa jimbo la Kyerwa, Bw. Inoncent Bilakwate pamoja na mbunge wa
viti maalumu mkoa wa Kagera Bibi Oliver Semnguruka walimuomba Waziri
Mkuu awasaidie katika uboreshwaji wa huduma za maji na afya.
Bw.
Bilakwate alisema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji
wa miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni tatu katika
jimbo hilo, lakini ujenzi wake hauridhishi, hivyo alimuomba Waziri Mkuu
awasaidie.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 7, 2018.
No comments:
Post a Comment