Mwanariadha Mourice Masima kutoka
Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza
kwenye mbio za KM 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza leo baada
ya kutumia muda wa saa 2:19:14. Kivutio
katika mbio hizo ilikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella ambae licha
ya kuzindua mbio hizo, alikimbia kikamilifu mbio za KM 42 akiambatana na baadhi
ya viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Magu Dk. Philemon Sengati.
Mwanariadha
Emmanuel Giniki kutoka Tanzania akimaliza katika nafasi ya kwanza
kwenye mbio za Kilometa 21 Rock City Marathon zilizofanyika jijini
Mwanza jana, baada ya kutumia muda wa 1:04:09 akifuatiwa na Mkenya
Daniel Kayioki aliyetumia muda wa saa 1:04:47.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John
Mongella katikati akishiriki katika mbio
za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika leo jijini Mwanza.
Mwanariadha
Mourice Masima Kutoka Kenya leo ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42
Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza huku Mtanzania Emmanuel Giniki
kutoka Tanzania akifanikiwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo
baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za km 21.
Katika mbio za km 42, Masima
alitumia muda wa saa 2:19:14 akifuatiwa na mshiriki mwenzake kutoka Kenya ,
James Emuria alietumia muda wa saa 2:19:58 wakati katika mbio za km 21, Giniki
alitumia saa 1:04:09 akifuatiwa na Mkenya Daniel Kayioki alietumia muda wa saa
1:04:47.
Kivutio
katika mbio hizo ilikuwa
ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella ambae licha ya kuzindua mbio
hizo,
alikimbia kikamilifu mbio za km 42 akiambatana na baadhi ya viongozi
waandamizi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Magu Dk. Philemon
Sengati .
Nafasi ya tatu katika mbio za km
42 pia ilichukuliwa Mkenya Declerk Omary aliyetumia muda wa saa 02:20:00 wakati katika
mbio za km 21 mshindi wa tatu ni Mokua Edwini Kutoka Kenya.
Upande wa wanawake mshindi wa
kwanza mbio za km 42 ni Naomi Jepngetich
kutoka Kenya aliyetumia muda wa saa
02:44:19 huku Mtanzania Failuna Matanga kutoka Tanzania akiibuka mshindi wa
kwanza katika mbio za km 21 akifuatiwa na Beatrice Nyaboke kutoka Kenya alieshika
nafasi ya pili.
Washindi wa kwanza katika mbio za km 42 katika
mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya
tisa mfululizo jijini humo waliibuka na kitita cha Sh 4 milioni kila mmoja,
washindi wa pili Sh 2 mil na washindi watatu Sh Mil 1 huku washindi wa nne hadi
wa kumi wakipata kiasi cha laki 5 kila mmoja kwa wanaume na wanawake.
Kwa upande wa mbio za km 21 washindi
wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake walijinyakulia pesa
tasliu kiasi cha sh mil 3 kila mmoja, washindi wa pili kiasi cha sh mil 1 na sh
750 kwa washindi wa tatu huku washindi wane hadi wa kumi nao wakiambulia kiasi
cha laki 3 kila mmoja.
Wakizungumzia siri ya ushindi wao,
mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliowawezesha kukimbia bila
changamoto yoyote , walisema ni kujituma
kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika
michuano ya mwaka huu.
“Maandalizi ni mazuri na washiriki walikiwa wengi wenye ushindani na
ninashukuru Mungu nimefanikiwa kuibuka mshindi na hatimaye watanzania tumeweza kuibuka washindi katika
mbio za km 21,” alisema Giniki.
Katika mashindano hayo
ilishuhudiwa washiriki ambao pia ni wadhamini wa mbio hizo kutoka makampuni ya Puma Energy Tanzania, Tiper,Rock
City Mall, NSSF, Gold Crest, New Mwanza
Hotel, CF Hospital, Coca Cola, Metro Fm,
EF Outdoor, KK Security, Belmont
Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link wakishiriki kikamilifu
katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
zawadi kwa washindi, Mongella aliwapongeza
washiriki na waandaaji wa mbio hizo na kutoa wito kwa wadau mbalimbali
kushirikiana kwa pamoja ili kurejesha hadhi ya mchezo wa riadha nchini.
“Nitumie fursa hii kutangaza
rasmi kuwa kila mwisho wa wiki tutakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili
tujiweke sawa kiafya. Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye
michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza
vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.” Alisema.
Naye Mwenyekiti wa mbio hizo Bw
Zenno Ngowi alisema mbali na kusaidia
utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadha nchini hususani katika
ukanda huu wa Ziwa, mbio hizo pia zinalenga kutangaza utalii wa ndani kwa
kupitia michezo, huku akitoa wito kwa wadau wa utalii kuunga mkono mbio hizo
No comments:
Post a Comment