Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akiangalia majina ya watu wanaotuhumiwa
kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi
hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo
mbalimbali Visiwani Zanzibar.Wengine
kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Emmanuel Lukula, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh na Katibu wa Naibu Waziri, George
Mwansasu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea,
Wilaya ya Mjini Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na
wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali
Visiwani Zanzibar.Wengine kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh
Mohamed Saleh na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Zanzibar, Masoud
Mabalila. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Ally
Saleh Ally, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la
kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani
Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Mariamu
Said Ali, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la
kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani
Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Msaidizi wa Polisi,
Saleh Mohamed Saleh, akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini
Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni
jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika
maeneo mbalimbali Visiwani
Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni.
Na Mwandishi Wetu
Wananchi wa eneo la Sogea,
Wilaya ya Mjini Unguja wamemkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, orodha ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya
Visiwani Zanzibar.
Wananchi hao wamekabidhi orodha
hiyo baada ya Naibu Waziri Masauni kuwataka waorodheshe majina ya watu
wanaowafahamu wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo ambayo imekuwa ikiaribu
nguvu kazi ya Taifa na kusababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu katika sehemu mbalimbali
Visiwani humo.
Awali wakiwasilisha kero zao kwa nyakati tofauti wananchi hao waliiomba serikali kudhibiti biashara hiyo ya
dawa za kulevya kwani imekua ikishamiri kwa kasi Visiwani humo na
wakishangaa ukimya wa mamlaka husika kuacha biashara hiyo ikizidi kuleta
madhara katika jamii.
Akizungumza katika Mkutano huo
wa hadhara, Naibu Waziri Masauni amewaahidi wananchi hao kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na wauzaji
wa dawa za kulevya huku akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata watu wote waliotuhumiwa na uchunguzi uanze mara moja.
“Hatuwezi kama Taifa
tukawa na vijana ambao hawana faida katika jamii,
vijana ni nguvu kazi ya Taifa, tutahakikisha majina
yaliyoletwa hapa tunayafanyia kazi na
natoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na
nitahitaji ripoti hiyo ndani ya wiki mbili, haiwezekani watu wachache waharibu
nguvu kazi ya Taifa kwa maslahi yao binafsi na familia zao,” alisema Masauni
Akizungumza katika mkutano huo ,
Kamishna Msaidizi, Saleh Mohamed Saleh, aliwaomba wananchi kuzifikisha taarifa za uhalifu katika vituo vya Jeshi la Polisi au Serikali ya Mtaa ili hatua ziwe zinachukuliwa ili kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment