WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema
Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa wilaya ya
Nachingwea wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao,
hivyo amewataka wananchi waendelee kuiamini.
Ameyasema hayo leo (Jumamosi,
Novemba 17, 2018) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Namatula ‘A’ na kijiji cha Mtua ambao waliosimamisha msafara wa Waziri
Mkuu wakati akiekea Kata ya Kilimarondo wilayani Nachingwea.
“Serikaliya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Nachingwea ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.”
Waziri Mkuu amesemaSerikali
kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo,
itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji
safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
Amesema mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza
umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo
nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini
(REA).
“Rais
wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata
umeme tena kwa gharama nafuu, hivyo ametenga fedha nyingi
zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya
ya Nachingwea. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”
Pia
Waziri Mkuu ameesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia
gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu
tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
Awali,
Waziri Mkuu alimkabidhi Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiluka saruji tani
mbili na nusu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi
Mpiluka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2018.
No comments:
Post a Comment