HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 25, 2018

Vodacom yatoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha ya watoto njiti kambi ya wakimbizi Nyarugusu

 Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Jacquiline Materu, akikabidhi mashine na vifaa vya hospitali ya kambi ya Nyarugusu kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Titus Luguha, katika kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki. Vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh. Mil. 25 vimetolewa ili kuongeza juhudi za kuhakikisha watoto wanaozaliwa njiti katika kambi hiyo wanaishi. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel na Mkuu wa Kambi hiyo, Francis Chokola, (wa nne kushoto). (Na Mpiga Picha Wetu).
 Katibu tawala wa Wilaya ya Kasulu, Titus Luguha, akimfunika moja kati ya wakimbizi waliojifungua watoto njiti katika kambi ya Nyarugusu misaada iliyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kambi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyuma yake ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Bi Jacquiline Materu, Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel, Bi Doris Mollel na wageni na wauguzi wa hospitali hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Bi Jacquiline Materu akikabidhi misaada kutoka Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa Bi Beatrice, moja kati ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imechangia vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa hospitali hiyo ili kuongeza juhudi za kuhakikisha watoto wanaozaliwa njiti katika kambi hiyo wanaishi. 


NA MWANDISHI WETU, KIGOMA

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi ya Vodacom Foundation wakishirikiana na Doris Mollel Foundation wamechangia vifaa tiba vyenye thamani ya shillingi milioni 25 katika hospitali iliyopo kwenye kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma, ili kuongeza  juhudi za kuhakikisha watoto wanaozaliwa njiti katika kambi hiyo wanaishi.

 Hospitali hiyo hutoa huduma kwa Wakimbizi waishio kambini hapo na wale wa kambi jirani ya Mtendeli lakini pia wanajamii wanaoishi maeneo jirani na kambi hizo.

Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka watoto millioni 15 huzaliwa kabla ya wakati yaani njiti kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo watoto milioni 1 hufariki kwa kukosa huduma muhimu. Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wambele kuchangia vifaa tiba katika vituo vya afya na hospitali hapa nchini ili kuokoa maisha ya watoto njiti.

“Watoto njiti wana nafasi kubwa ya kukua na kuwa na afya nzuri bila ulemavu endapo watapata msaada wa vifaa na usimamizi wa afya kuzingatiwa na ndio maana sisi kama Vodacom Tanzania Foundation tunafuraha sana kuwa sehemu ya wanaochangia kuhakikisha watoto njiti nchini wanaishi” alisema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mahusiano Bi Jacquiline Materu huku akiongeza kwamba Vodacom Tanzania Foundation imejikita katika kuboresha huduma za afya na elimu kwa Wanawake pamoja na watoto nchini Tanzania.


Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya serikali  mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dk. John Jingu, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Titus Mguha, alizishukuru taasisi za Vodacom Tanzania Foundation na Doris Mollel kwa kuunga juhudi za serikali za kuokoa maisha ya watoto “Msaada huu umekuja  ndani  ya muda muafaka wakati ambapo serikali imezindua kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama kuhamasisha watu na Taasisi mbali mbali kupigania kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

 Nina furaha kubwa kuona muungano huu wa Vodacom Tanzania Foundation na Doris Mollel Foundation ukifanya kazi kuboresha afya ya watoto na mama katika kambi hii,”alisema.

Kwa upande wake, mratibu wa afya katika kambi ya Nyarugusu Dr Athumani Juma  alisema hospitali hiyo imekuwa  na changamoto ya kusaidia maisha ya watoto njiti wanaozaliwa hapo hospitalini.

“Tumefanikiwa kukarabati wodi  ya watoto njiti lakini tulikuwa na changamoto ya vifaa hivyo tunashukuru sana kwa mchango huu wa vifaa vya kuokoa maisha ya watoto njiti wanaozaliwa hospitalini hapa na tunaahidi uangalizi wa karibu” 

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vifaa vya oksijeni (Oxygen concentrator) ambavyo vitasaidia watoto njiti kupumua, thermometers 10, 4 weighing scales for infants, 40branded bed sheets, baby warmer, 3 suction machines, ambu bag with facemasks for infants, 1000 feeding tubes, phototherapy machine, na vitanda vitatu vya watoto.

No comments:

Post a Comment

Pages