NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA
Mkoa wa Tabora
umeanisha maeneo ya vipaumbe vya uwekezaji katika kila Halmashauri nane za Mkoa
huo ambayo yatajengwa viwanda vikubwa na
uanzishaji wa ranchi kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe.
Kauli hiyo ilitolewa
hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa majumuisho ya
kikao cha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.
Alisema kwa upande wa
Wilaya ya Urambo wamepewa jukumu la kutenga eneo la ujenzi wa Kiwanda cha
Kusindika Tumbaku, Halmashauri ya Kaliua wapewa jukumu la kujenga kiwanda cha
mazao ya misitu.
Mwanri alisema Sikonge
wenye wanatakiwa kuandaa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuchakata mazao
ya nyuki ikiwemo asali na nta kwa ajili ya kuongeza ubora wake ili yaweze kupata soko kubwa ndani na nje ya
Nchi.
Alisema Halmashauri ya
Mji wa Nzega imepewa jukumu la kuwa na eneo kwa ajili ya machijio ya nyama na Kiwanda
cha kuchakata nyama ya ng’ombe na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega inapewa jukumu
la kuandaa na kuanzisha Rachi kwa ajili
ya kunenepesha ng’ombe ili kuwezesha kuwa na nyama nzuri itakayopata soko ndani
na nje ya Nchi.
Mwanri alisema Igunga
wamepewa jukumu la kuimarisha kilimo kikubwa cha pamba kwa ajili ya viwanda
Tabora na Manonga na kuongeza maeneo ya miradi ya umwagiliaji mpunga, ujenzi wa
viwanda vya kukoboa mpunga ambavyo vitasaidia kuuweka katika madaraja.
Alisema Uyui watahusika
zaidi kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya
alizeti na mazao mengine.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema kuwa Manispaa ya Tabora wanatakiwa kutenga eneo kwa ajili ya ukanda maalumu
wa uwekezaji ambapo vitajengwa viwanda kama vile wa EPZA Ubungo Jijini Dar es salaam.
Alisema Mkoa umefikia
uamuzi huo ili kutogawanya nguvu na kufanya baadhi ya viwanda kushindwa kufanya
kazi vizuri kwa sababu ya uchache wa malighafi kutokana na kuwepo kwa mrudikano
wa viwanda vya aina moja katika eneo moja.
No comments:
Post a Comment