*Ni dhiri ya wanawake na watoto katika jamii kwa silimia 50 ifikapo 2022
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amesema Serikali imeandaa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza kiwango cha
ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii kwa asilimia 50 ifikapo
mwaka 2022.
Amesema
mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na
Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya
Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA
(1998).
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 25, 2018) wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsiakatika
Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Amesema katika kukabialia na ukatili
wa kijinsia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli imekuwa ikichukua hatua mbalimbaliza kuzuia na kutokomeza
ukatili.
Waziri
Mkuu amesema utekelezaji wa mpango huo utachangia katika utekelezaji wa
mipango na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia,
uwezeshaji wanawake na wasichana pamoja na haki na ustawi wa mtoto.
Kadhalika
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote
wahakikishe wanasimamia uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na
Watoto za ngazi za Mikoa, Halmashauri, Kata na Vijiji kama
inavyoelekezwa katika Mwongozo wa uratibu wa Mpango wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
“Vilevile,
nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuanzisha Programu za
Kijamii za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Halmashauri husika
zitakazozingatia hali halisi na kuzitengea bajeti programu hizo kama
inavyoelekezwa kwenye Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi
ya Wanawake na Watoto. “
Pia Waziri Mkuu amesema watu
wenye ulemavu wana mahitaji maalumu na ni wahanga wa ukatili wa
kijinsia ameelekeza Jeshi la Polisi kuboresha Dawati lake la jinsia ili
liweze kushughulikia kikamilifu masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya
watu wenye ulemavu. “Hivyo, kuanzia sasa Dawati hilo liitwe Dawati la
Polisi la Jinsia, Watoto na Watu wenye Ulemavu.”
Akizungumzia
kuhusu maana ya ukatili wa kijinsia amesema ni hali ya kutenda vitendo
viovu, vinavyodhalilisha, vinavyotesa, vinavyonyanyasa,
vinavyokandamiza, visivyojali haki za kuishi kwa binadamu anaweza kuwa
wa kiume au kike.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema ukatili wa kijinsia huja katika taswira nyingi.
“Aidha, kwa uchache tunapozungumzia ukatili wa kijinsia tunamaanisha
vitendo kama vile, vipigo, ubakaji, ukeketaji, ulawiti, matusi, lugha na
vitendo vya udhalilishaji pamoja na kunyimwa fursa za kushiriki katika
shughuli za kiuchumi.”
“Hivyo,
ukatili wa kijinsia ni unyanyasaji wowote unaofanywa na mtu dhidi ya
mtu mwingine bila kujali umri, maumbile, kabila, rangi, dini au mtazamo
wa kisiasa. Unyanyasaji huu unahusisha mambo mengi kama kumpiga mwanamke
au mwanamme, kumnyima mtoto elimu, kumlawiti mtoto wa kike au kiume,
kumbagua mtu katika mahitaji ya msingi au kuwanyima urithi warithi
wanaohusika.”
Aidha, taarifa kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) za mwaka 2017 zinaonesha kuwa
wanawake na wasichana wapatao milioni 750 Duniani waliolewa wakiwa
chini ya miaka 18. Halikadhalika, taarifa hiyo inakadiria kuwa wasichana
milioni 120 (yaani mmoja kati ya wasichana 10) Duniani wamekumbana na
vitendo vya kulazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao.
Waziri
Mkuu amesema kama zilivyo nchi nyingine Duniani, Tanzania ni miongoni
mwa nchi ambazo zinakabiliwa na tatizo la ukatili wa kijinsia na kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka
2015/2016 kupitia inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri
kati ya miaka 15 - 49 wamefanyiwa ukatili wa kupigwa au kingono katika
kipindi cha maisha yao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPilI, NOVEMBA 25, 2018.
No comments:
Post a Comment