HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 03, 2018

11 of 134 Shule Binafsi zatakiwa kufuata mitaala

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka Wamiliki wa shule binafsi kufuata sheria na Miongozo ya Elimu ikiwemo kufuata Mitaala ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu inayoendana na ukuwaji wa sayansi na Teknolojia.

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri katika Sherehe za kukamilika mwaka wa masomo katika Shule ya Turkish Maarif Foundation inayosimamiwa na Serikali ya Uturuki iliopo kidimni Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema ni vyema kwa wamiliki hao kufuata mitaala ilipo ili kuinua kiwango cha elimu Nchini ikienda sambamba na mfumo uliopo ili isiwepo tofauti baina ya shule za Serikali binafsi.

“Sasa nyinyi kazi yenu ubunifu ili kuwapa watoto wetu vitu vilivyo bora ambapo vitawashawishi wazazi wengine kuleta watoto wao” alisema Naibu.

Aidha Naibu Mmanga aliutaka uongozi wa shule hiyo kubuni mbinu bora za ufundishaji ambazo zitawawezesha wanafunzi kuweza kuendelea na elimu ya juu baada ya kukamilika masomo yao ya sekondari.

Hata hivyo ametowa wito kwa Walimu na Wanafunzi kufuta Sheria na maadili ilikujiepusha na Vitendo vya Udhalilishaji wa kijinsia ambavyo vitapelekea kushusha mamendeleo ya Elimu Nchini.

Akisoma risala kwa niaba ya shule hiyo mwanafunzi Muhamed Abdul aziz Wameiomba Serikali kuharakisha Usajili wa kituo cha kufanyia mitihani Katika Skuli hiyo ili waweze kuungana pamoja na Skuli nyengine katika Mitihani ya Taifa hapo mwakani.

Pia Mkurugenzi wa shule Hassan Issa Ali alieleza kuwa wanakabiliwa na tatizo la kukatika Umeme na kupelekea vifaa vyao ikiwemo Computer kuungua jambo ambalo linawapa hasara kubwa kwa ununuzi wa vifaa hivyo mara kwa mara.

Aidha aliliomba Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) kuangalia namna ya kuwatatulia tatizo hilo ili waweze kunufaika na huduma ya umeme katika skuli hiyo.

Wakati huo huo Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Ali Davotuglu alieleza Serikali ya uturuki itaendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar katika kuwaletea maendeleo wananchi hususan katika sekta ya elimu ambayo inatowa miongozo bora kwa wanafunzi.

Balozi Davotuglu amesisitiza uongozi wa Shule hiy kuthamini na kujua juhudi za utoaji wa elimu bora ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa ikiwemo kuengeza wataalamu wenye viwango Nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages