HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 04, 2018

Halotel, Biko kunogesha michezo msimu wa sikukuu

 Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Halotel, Nguyen Huu Hanh,  wakisaina makubaliano ya kushirikia katika mchezo kwa ajili ya kunogesha msimu wa sikukuu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven (kushoto), na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Halotel, Nguyen Huu Hanh,  wakibadilisha makabrasha baada kusaini makubaliano ya kushirikia katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kwa ajili ya kunogesha msimu wa sikukuu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu makubaliano ya kushirikia katika michezo ya kubashiri kwa ajili ya kunogesha msimu wa sikukuu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu makubaliano ya kushirikia na halotel katika michezo ya kubashiri kwa ajili ya kunogesha msimu wa sikukuu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Halopesa, Magesa Wandwi, akizungumza katika hafla hiyo.

 Baadhi ya waandishi wa habari.


NA FRANCIS DANDE

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Halotel Tanzania, imeingia katika makubaliano rasmi na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha na Kubashiri ya Biko Tanzania ili kuongeza msisimko na ushiriki kwa wadau wa michezo hiyo nchini katika msimu huu wa sikukuu.

Ushirikiano huo utawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel kupitia huduma ya kifedha ya HaloPesa kupata fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko Tanzania kwa kubahatisha na pia kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali na Bikosports.

Akizungumza waandishi wa habari makao makuu ya Ofisi za Halotel, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda alisema, “Ushirikiano huu baina ya kampuni yetu na Biko utawawezesha wateja wetu kuweza kushiriki na kupata fursa ya kujishindia fedha zitakazowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

“Mtandao wetu na huduma ya Halopesa imeenea nchi nzima katika maeneo ya mjini na vijijini, jambo ambalo sasa litatoa fursa mpya ya ushiriki katika michezo kwa wateja wetu walioko nchi nzima, ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa hawapati fursa hii ya kushiriki. Tunaamini sasa wateja wetu walioko nchi nzima wataweza kushiriki katika michezo ya kubashiri na kubahatisha kupitia Biko Tanzania”. Aliongeza Semwenda.

“Hii ni fursa kwa wateja wetu wote wa Halotel mijini na vijijini kuweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kama vile mpira wa miguu, mpira wa kikapu, Rugby, Cricket, Tennis na mingineyo ambapo hapo kabla hawakuweza kupata fursa kushiriki katika michezo hii kwa kupitia mtandao wa Halotel (HaloPesa) kwa kutumia namba USSD za Halopesa ambazo ni (*150*88#) wenye mawakala zaidi ya elfu 55,000. Alihitimisha Semwenda.

Aidha kwa upande wake, Meneja Masoko Biko Goodhope Heaven alisema “Hii ni nafasi ya muhimu kwetu na kwa wateja wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Halotel Tanzania kwa kupitia huduma yao HaloPesa.  Kama mnavyojua, Biko ni kampuni kubwa na madhubuti inayojihusisha na michezo ya kubahatisha kwa kufanya miamala kwenye simu za mkononi ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456 au sawa na neno biko. 
Mbali na hilo, pia tunaendesha mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ujlikanao kama bikosports.

“Wateja wa HALOTEL wanatakiwa kufanya miamala kwenye simu za mkononi ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456 au sawa na neno biko kwa kupiga namba *150*88#, kuchagua lipa bili na Halopesa, kisha chagua 4: Michezo ya kubahatisha ambapo namba 5 ni Biko (505050) kisha namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, kisha ataweka kiasi pamoja na namba ya siri ili kukamilisha muamala”. Alisema Heaven.

“Kampuni yetu ilianza mapema mwaka jana na imekuwa ikihusisha watu wanye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea. Tangu wakati huo, watu wengi wameneemeka kwa kushinda zawadi za fedha, pikipiki na nyumba. Aliongeza Heaven.

Ushirika na Halotel umekuja wakati muafaka ambapo wateja wa Halotel kupitia Biko Tanzania sasa watapata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia zawadi mbalimbali kutoka BIKO MSHIKO NJE NJE.

No comments:

Post a Comment

Pages