HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 04, 2018

JPM ateua makamishna wa tume ya utumishi wa umma

NA TATU MOHAMED

RAIS Dk.  John Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Steven Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 3.

Pamoja na kumteua mwenyekiti wa tume, Magufuli amewateua Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa uteuzi huo wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma umeanza tangu Novemba 22, 2018.

Aliwataja makamishna walioteuliwa kuwa ni George Yambesi, Balozi Mstaafu John Haule, Immaculate Ngwale, Yahaya Mbila pamoja na  Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay.

No comments:

Post a Comment

Pages