HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2018

TAMASHA LA TIGO FIESTA KUFANYIKA VIWANJA VYA POSTA DAR


Mkuu wa Kitengo cha  Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga (wa pili kushoto), akiwa na mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018 Gardner Habash (wa pili kulia), pamoja na baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 litalaofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Msanii  Nedy Music (kushoto),  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Posta jinjini Dar es Salam Jumamosi.  Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo Huduma za  wa Tigo Masoko William Mpinga akifuatiwa na Mratibu wa tamasha hilo GardnerHabash kutoka Clouds Media Group akifuatia na msanii Chege.

Dar es Salaam, Tanzania

 Kilele cha Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote kinatarajiwa kuwaenzi ‘championi’ wote waliofanikisha msimu huu wa kipekee, wakati wasanii 100% wa nyumbani watakaposhuka jukwaani kuhitimisha msimu huu siku ya Jumamosi katika viwanja vya Posta – Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

“Ningepeda kuwashukuru championi/ mabingwa wote waliokuwa sehemu ya mafanikio ya msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, nikianza na maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika mikoa yote 14 kuwapa sapoti wasanii wetu wa ndani,”  Mkuu wa Huudma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema.

Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardber Habash alisema,  ‘Msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote umetimiza lengo lake la kuinua viwango vya mziki na kukuza vipaji vya wasanii wa Kitanzania ili waweze kushindana katika soko la kimataifa.”

Aliongeza kuwa wafanyabiashara pamoja na viongozi wa serikali katika maeneo yote yaliyokuwa sehemu ya msimu huu walifurahia fursa za biashara na kukuza vipato zilizotokana na Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote. “Tunawashukuru watendaji wote wa serikali pamoja na wafanyabiashara wakubwa na wadogo waliojitokeza kuwa machampioni kwa kusaidia kufanikisha tamasha hili pamoja na kuchamgakia fursa za biashara zilizojitokeza,” alisema.

Kuelekea kilele cha msimu huu mkubwa zaidi wa burudani katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kampuni ya Tigio imetangaza punguzo kubwa la bei kwa tiketi zote zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa/Masterpass QR.

‘Kama njia mojawapo ya kuwashukuru championi wote wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Tigo inatoa punguzo kubwa la zaidi ya asilimia 30% kwa tiketi za tamasha la Dar es Salaam zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa/Masterpass QR. Tiketi za tamasha hilo zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 10,000 kupitia Tigo Pesa/Masterpass QR badala ya bei ya TSH 15,000 itakayotumika kwa tiketi zitakazonunuliwa mlangoni,’ William Mpinga aliwaambia waandishi wa habari.

Ili kupata ofa hiyo ya tiketi, wateja wa Tigo wanapaswa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), kubonyeza 2 (lipa Masterpass QR) na kisha kutuma gharama husika ya TSH 10,000 pekee kwenda kwa namba ya Tigo Fiesta 78888888. Ofa hii pia ipo wazi kwa watumiaji wa mitandao mingine wanaopaswa kufuata hatua za kawaida wanazotumia kutuma pesa katika mitandao husika.

‘Kila wanaponunua tiketi kwa njia ya Masterpass QR, wateja wa Tigo pia wanajiongezea nafasi ya kushinda TSH 1 milioni kila siku, TSH 10 milioni kila wiki ama hadi TSH 50 milioni katika promosheni kubwa ya Jigiftishe inayotoa zawadi za pesa taslim katika msimu huu Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya,’” William aliongeza. Promosheni hiyo kabambe ya Jigiftishe inawazawadia wateja kwa kutumia huduma za Tigo, bila masharti yoyote wala ulazima wa kujiunga na promosheni yenyewe.

Baada ya kuzuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linahitimisha mwaka wake wa 17 huku likiwa limetimiza ahadi yake ya kukuza viwango vya muziki wa nyumbani na kukuza wasanii wa ndani ili wafikie viwango vya kimataifa.

Wafanyabiashara pamoja na viongozi wa serikali katika mikoa yote iliyoshuhudia tamasha hilo mwaka huu wamepongeza mchango mkubwa wa Tigo Fiesta 2018 katika kuibua fursa za biashara katika maeneo husika. Wafanyabishara waliofaidi zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaohudhuria tamasha hilo ni pamoja na wamiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni, migahawa na mama nitilie, wenye maduka, wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki wa vyombo vya usafiri kama daladala na bodaboda pamoja na watoaji wa huduma nyingine mbalimbali.  Fursa nyingi zaidi za biashara zinatarajiwa kuibuliwa katika tamasha la kufunga msimu jijjni Dar es Salaam litakaloanza saa kumi na mbili jioni hadi majogooo.

Waandaaji Clouds Media Group kupitia Katibu Mkuu Kiongozi wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash wamebainisha kuwa tamasha la kufunga msimu litashuhudia wasanii wanaochipuka kutoka mikoa 14 ya nchi wanaoshiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 Supa Nyota wakipanda jukwaani kutuo burudani kuwasindikiza wasanii wakongwe wa bongo flava. “Kufikia sasa tuna wasanii zaidi ya 30 watakaotumbuiza katika tamasha la Dar es Salaam na tunazidi kusajili wasanii wengine kwa hiyo wapenzi wa muziki wajiandae kupata shoo kali na vibes za uhakika Jumamosi hii,’ Gardner alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages