WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali imeanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa lengo la
kuwasaidia wakulima wapate mitaji ili waongeze tija.
Pia
amewataka wakuu wa wilaya za Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro
wahahakikishe wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuchangamkia
fursa ya kilimo cha miwa.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipotembelea
shama la miwa Mkulazi na MbIgiri mkoani Morogoro alipokuwa njiani kwenda
jijini Dodoma.
Alisema
lengo la kuanzishwa shamba la mwa la Mkulazi ni katika jitihada za
Serikali za kuhakikisha mahitaji ya sukari nchini yanafikikia katika
kiwango kinachohitajika.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imepanga kuzalisha sukari itakayotosheleza
mahitaji na njia pekee ni kuboresha kilimo cha miwa, kujenga viwanda
vitakavyozalisha sukari ya kutosha.
Alisema
shamba hilo linaendeshwa kwa ubia kati ya NSSF na Jeshi la Magereza,
hivyo, aliiagiza Menejimenti mpya ya Mkulazi kuhakikisha shamba hilo
linasimamiwa kikamilifu.
Waziri
Mkuu pia, alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
apeleke wataalamu wengi wa kilimo katika shamba hilo ili wasaidie
kusimamia kitaalamu.
“Nataka
shamba hili lisimamiwe kitaalamu, uzalishaji uwe wa kitaalamu na liwe
mfano na mashamba mengine, tusishindwe na watu binafsi,” alisema.
Kuhusu
suala la maji hususan kipindi cha mvua ambayo huaribu shamba, Waziri
Mkuu aliwataka watafute namna nzuri ya kuyahifadhi ili wayatumie kipindi
cha kiangazi.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka watafute mashine nyingine zitakazotosha
kumwagilia shamba hilo wakati wa kiangazi ili miwa isiharibike na
iendelee kuwa ya kijani wakati wote.
Nae,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenistar Mhagama, alisema shamba la Mkulazi II ni miongoni mwa
mashamba mawili yanayomiilikiwa na wabia wawili yaani NSSF na Jeshi la
Magereza.
Alisema
walikubaliana wao na Magereza wafanye kazi kwa kuongozwa na uzalendo,
maadili ya utendaji wa kazi, uaminifu ili mwisho wa siku mradi huo uwe
na tija na uweze kuwafikisha katika malengo yaliyokusudiwa.
Alisema
wanaamini fedha zilizowekezwa kwenye mradi huo ambazo ni za wanachama
zinatakiwa zirudishe faida kwa wanachama wenyewe na kujenga uchumi wa
Taifa.
Kwa upande wake,
Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba, alimshukuru Rais Dkt. John
Magufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha tatizo la upatikanaji
wa sukari nchini linakuwa historia.
Alisema
mbali ya shamba hilo la Mkulazi II pia kuna lingine la Mkulazi I ambalo
ni kubwa zaidi, hivyo alishauri liendelezwe ili limalize tatizo la
sukari nchini. Waziri Mkuu alimtaka ashughulikie shamba hilo kwa kuwa
lipo Wizara ya Kilimo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, DESEMBA8, 2018.
No comments:
Post a Comment