Na Talib Ussi, Zanzibar
Umoja wa mataifa (UN) imeeleza inawezekana kuwa na taifa bila ya
udhalilishaji wa wanawake na watoto, jambo ambalo ni kero kubwa katika jamii
mbali mbali Tanzania na Duniani kote.
Akizungumza
kwa niaba
ya mashirika ya UN katika maadhimisha ya siku 16 za kupambana na
udhalilishaji
wa wanawake na watoto zilizofanyika Visiwani Zanzibar katika Ukumbi wa
Sheikh Idrisa Abdul-Wakili, Alvaro Rodriguez (Pichani), alisema inasikitisha kuona
kwamba bado
katika jamii nyingi Duniani udhalilishaji unaendelea.
“Tunaweza kutokomeza
vitendo hivi viovu kwa kila mmoja kutekeleza wajibu wake , tuungane ili akina
mama waishi bila ghofu” alisema Rodregues alisema tamko la Un kuhusiana na siku
16 kupinga ukatili wa kijinsia.
Alieleza kuwa maendeleo
ya wanawake hayawezi kufikiwa ikiwa jamii zilizonguka bado zinaendelea na
udhalilishaji.
“Udhalilishaji hauvumiliki
ni lazima tutapambane nao kwa hali yoyote ile kwa maslahi ya jamii iliyobora”
alieelza mwakilishi huyo wa un.
Aidha aliomba jamii
kuwafariji wahanga wa vitendo hivyo na kuchukuliwa hatua kali kwa wahalifu
wanaotenda vitendo hivo.
Kwa upande wake Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi zanzibar Balozi Seif Ali Idd amewataka wanawake
kutokuogopa kuachwa na waume zao (kupewa talaka) kwa kuwaficha wahalifu wa
vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Balozi alieleza kuwa
wapo baadhi ya wanwake kutotoa taarifa au kuwaficha wadhalilishaji kwa kuogopa
kuachwa au kupewa talaka na waume zao jambo linasababisha vita dhidi ya
udhalilishaji kuwa ngumu.
“Kama mwanamke ukificha
vitendo vya udhalilishaji basi mtoto wako akiendelea kufanyiwa udhalilishaji
usipige kelele, ni vyema sote tukashirikiana kuliondoa janga hili” alieleza
Balozi Seif.
Sambamba na hilo Balozi
alieleza kuwa kutokomeza kabisa jambo hilo ni lazima kuwepo nguvu ya pamoja
baina ya jamii, Wanasheria pamoja na Serikali.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi zanzibar Khamis Mwinyi Muhammed alisema taasisi
yake imekuwa ikipiga siku zote suala la udhalilishaji.
“Tulinde nguvu kazi
tumalize udhalilishaji wa kijinsia sehemu za kazi” alieelza katibu huyo ambao
huo ni ujumbe mwaka huu.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara ya ya Kazi, Uwezeshaji Wazee wanawake na Watoto zanzibar Bi
Fatma gharib Bilali alisema wazara yake imezifanyia mabadiliko sheria nyingi
ambazo zinahusiana na vitendo hivyo kwa lengo kuziba mwanya wa kutokea kwa
watendaji wa laana hiyo.
Alieleza kuwa katika
sheria ya ajira namba 11 ya 2015
imewataka taasisi binafsi kupambana na udhalilishaji katika maeneo yao ya kazi.
“Tumeamua kufanya
sheria kali ili kuwadhibiti wahalifu wa vitendo hivi na kwa sasa hawatakiwi
kupewa dhamana” alieleza Bi Fatma.
Dunia huazimisha siku
16 kila mwaka kwa lengo la kuongoza
mwamko wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji.
No comments:
Post a Comment