Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri
Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio wakati wa
ziara yake katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Denge Beach Kigamboni Jijini Dar
es Salaam Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
NA
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mhe.Waziri Mhagama ameuagiza uongozi wa Shiriki la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF) kubadili mitazamo dhaifu ya kiutendaji na kuanza kufanya kazi kwa
kuongozwa na uzalendo ili kuleta tija na kufikia malengo ya Shirika hilo.
Ametoa kauli hiyo mapema
mwishoni mwa wiki hii (Novemba 29, 2018) alipofanya ziara ya kukagua
utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba
za bei nafuu Dar es Salaam.
Maeneo aliyotembelea ni
pamoja na; miradi wa nyumba za bei nafuu za Dungu, Mtoni Kijichi, Tuangoma na
Mzizima pamoja na nyumba za Dege Beach Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Kauli ya waziri
imekuja mara baada ya kutoridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa miradi
hiyo na kuuagiza uongozi wa Shirika hilo kubadili mitazamo ili kuwa na malengo
yanayotekelezeka na kwa wakati.
“Kwa muda mrefu mmekuwa
mkifanya kazi kwa kujitenga katika makundi, mnapaswa kubadili mitazamo hasi na
kuwa na mitazamo chanya yenye utendajikazi katika hali ya umoja ili kuendelea
kubadili NSSF ili iwe na uzalizaji wa tija”.alieleza Mhagama
Waziri aliongezea kuwa
Shiriki linapaswa kubadili hali za mazoea yaliyokuwa si mazuri ili kuendana na
kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano iliyojikita katika uwajibikaji wa kizalendo.
“Lazima mbadili mitazamo ya
uongozi wa mazoea na kuanza kufanya kazi
kwa umoja ili kuwa na matokeo chanya yanayokusudiwa ili kuwa na tija kwa jamii
na Serikali kwa ujumla”.Alisisitiza Mhagama
Sambamba na hilo waziri
alielekeza uongozi wa NSSF pamoja na bodi
kuanza kuchukua hatua kwa watendaji wazembe pasipo uwoga katika kuongoza
kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
“Niwaombe Uongozi wa Shirika
pamoja na Bodi mfanye kazi mkiongozwa na sheria, kanuni na taratibu zilizopo,
mahali pa kuchukua sheria, tuone mkifanya hivyo bila kuoneana aibu”.Alisisitiza
Waziri
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii wa NSSF Bw.William Erio aliahidi kuchukua
maelekezo ya waziri kwa vitendo na kuanza utekelezaji wa haraka juu ya maeneo
aliyoelekeza.
“Niahidi kwa kushirikiana na
menejimenti na bodi kuendelea kuweka mipango inayotekelezeka na kuhakikisha tunawajibika
ili kuwa na NSSF yenye sura mpya”.Alisema Erio
Naye mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya mfuko huo Balozi Ali Iddi Siwa aliahidi kutekeleza maagizo
yaliyotolewa na kuhakikisha waneendelea kuhakikisha shirika linakuwa katika
viwango vya juu kama matarajio ya Serikali juu ya NSSF.
“Nikuhakikishie kuwa
tutafanya yale yote uliyoagiza ili kuendelea kulitangaza vyema Shirika na kuhakikisha kazi zote za Bodi
zinatekelezwa vyema kwa kuzingatia utawala bora wenye weredi na
uzalendo”.Alisisitiza Balozi.
AWALI
Miradi ya Ujenzi wa Nyumba
za Bei nafuu ya eneo la Mtoni Kijichi, Tuangoma, Mzizima na Dege ilianza kutekelezwa
mwaka 2013 hadi sasa.
Mradi wa Dungu una jumla ya
nyumba 439, mradi wa Tuangoma una jumla ya nyumba 161, Denge una jumla ya
nyumba 3750, Kijichi jumla ya nyumba zaidi ya 820 pamoja na miradi hiyo,
shirika limejenga jengo la ghorofa refu lenye Jumla ya Ghorofa 35 lililopo eneo
la Mzizima Posta Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment