HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 15, 2019


 Mfalme wa Sokoto (Nigeria) na Kabaka wa Bunganda Bugunda (Uganda) watoa wito kwa viongozi wa kijadi na dini kuungana katika jitihada za kuwabakiza wasichana shuleni

Kusanyiko la viongozi kutoka barani kote lahimiza jitihada ya kuwabakiza wasichana shuleni

Abuja, Nigeria, Januari, 15 2019 – Sultani wa Sokoto (Nigeria), Mtukufu Muhammadu Sa’ad Abubakar III, pamoja na Kabaka wa Bugundu (Uganda), Mtukufu Ronald Edward Frederick Kimera Muwenda Mutebi II, leo, wataongoza ‘Mkutano Mkuu wa Kuwabakiza Wasichana Shuleni’; ambao unawaleta pamoja huko Abuja, Nigeria viongozi wa Kiafrika, watawala wa jadi, viongozi wa kidini, makundi ya vijana, watetezi na wajenga hoja. 

Tukio hilo la litakalodumu kwa siku mbili litawaleta pamoja viongozi wa kimila na kidini wenye ushawishi mkubwa kutoka kote barani ili kujadili suala muhimu la kuwabakiza wasichana shuleni ili wasikatishe masomo yao ya elimu ya msingi na ile ya sekondari (yaani, miaka 12 ya elimu) na kutafuta masuluhisho kutoka mingoni mwa wajenga hoja hodari wa Kiafrika kutoka tamaduni na amali tofauti. Huku umaskini ukiwa ni miongoni mwa masuala yanayosababisha wasichana kukatisha masomo, Mkutano Mkuu huo pia unataka kuhamasisha uingizwaji wa stadi mbalimbali katika mfumo wa elimu ili kuingiza kipato.

Kwa miongo kadhaa, serikali za Kiafrika na washrika wa kimataifa wa maendeleo wamefanya jitihada za kujaribu kuimarisha na kupunguza mateso yanayotokana na ujauzito na uzazi wa utotoni. 

Kumekuwa na mafanikio kidogo katika afya ya wanawake na watoto, licha ya tafiti kuonyesha kwamba afya ya watoto huwa bora zaidi pale mama anapokuwa na elimu zaidi. Kukamilisha elimu ya sekondari kwa wasichana limeonekana kuwa ni jambo muhimu linaloimarisha si tu afya ya mama na mtoto bali uwezo wa wanawake wa kufanya maamuzi, na pia uwezo wao wa kujipatia riziki; kwa hiyo kuwa na matokeo bora katika afya na lishe ya familia na jamii. Uhusiano usiopingika kati ya elimu ya mama na matokeo ya kimaendeleo ya familia, unaonyesha kwamba hatma ya familia za Kiafrika inategemea elimu ya mtoto wa kike.

Mkutano huo mkuu utatoa jukwaa ambamo kwamo viongozi wa kijamii watabadilishana mawazo na njia bora na kuandaa mikakati na mitandao ya kuwabakiza wasichana shuleni. Pia ni njia ya kujenga welewa na kuwapa viongozi ujuzi sahihi wa kuwahamasisha wazazi na walezi kujitolea zaidi ili kuhakikisha wasichana wote katika majibo yao walau wanakamilisha miaka 12 ya safari ya elimu.

Akizungumza katika tukio hilo, Sultani wa Sokoto, Mtukufu Muhammadu Sa'ad Abubakar III alitoa wito ka viongozi wote wa kijadi na kidini barani Afrika kuweka mkazo katika maendeleo ya jamii zao; akisema, “Suala muhimu katika maendeleo ya jamii zetu ni elimu kwa watoto wetu wa kike.”
Aliongeza kusema: “Ninaamini viongozi wa kijadi na kidini wataongoza katika kujenga hatma mpya ya Afrika kwa kuhakikisha wasichana wote wanamaliza elimu ya sekondari na kujifunza stadi za maisha na za kujipatia kipato katika mchakato huo wa elimu.” 

Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na Mheshimiwa Muhammadu Buhari, Rais wa Jamhuri ya Kifederali ya Nigeria, Mtawala (Emir) wa Kano (Nigeria) Mtukufu Muhammadu Sanusi II ambaye aliwasilisha ripoti kuu ya utafiti iliyopewa kichwa cha habari cha “Mitazamo kuhusu Maendeleo Barani Afrika—idadi ya watu, elimu na uwekezaji” (“Perspective on Development in Africa - population, education and investment”); Mtawala (Emir) wa Argungu (Kebbi state, Nigeria) Mtukufu Alhaji Samaila Mer Malkia, Nnabagereka wa Buganda Malkia Sylvia Nagginda; Mtawala (Asantehene) wa Asante Ghana,; Askofu Mkuu wa Abuja, Kardinali John Onaiyekan; Sheikh Sheriff Ibrahim Saleh; Mama wa Malkia wa Asante, Mtukufu Nana Ama Konadu; Sultani wa Zinder (Jamhuri ya Niger) Mtukufu Al-hajj Aboubacar Sanda na pia wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa kama vile Taasisi ya Mfuko wa Uwekezaji wa Watoto (Children’s Investment Fund Foundation (CIFF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) la Nigeria, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Uingereza (DFID) na mengineyo. Pia, miongoni mwa walioshiriki walikuwa ni wawakilishi kutoka katika wizara, idara na wakala mbalimbali wa Nigeria wakiwemo Waziri wa Jimbo Kuu la Kifederali la Makao Makuu (FCT), Muhammad Musa Bello na Waziri wa Elimu Mallam Adamu Adamu, ambaye katika hotuba yake fupi alisisitiza umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike. 

Mkutano huo mkuu uliwapa fursa viongozi wa kijadi na kidini walioshiriki kutafakari na kuibua mawazo juu ya namna wanavyoweza kuchangia katika kampeni/vuguvugu la kuwabakiza wasichana shuleni katika jamii zao kwa kuongeza idadi ya wanaoandikishwa, kuwabakiza shuleni na kumaliza elimu yao na pia kuhakikisha wasichana wanapata stadi za maisha na kujikimu. Juhudi hii itapewa nguvu zaidi kupitia misaada kwa vikundi vya jinsia na vijana na taasisi zao.

Makundi ya Vijana wa Kiafrika yatawasaidia viongozi wa kijadi na kidini kwa kutangaza zaidi juhudi hizi kupitia kuwahamasisha vijana kuiga na kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha kampeni ya Kuwabakiza Wasichana Shuleni katika jamii zao. Juhudi hizi pia zinawaleta pamoja viongozi wanawake wa Kiafrika ambao watatumia ushawishi wao kuhamasisha kuwabakiza wasichana shuleni, wakiwa kama watu wa kupigiwa mfano na viongozi katika jamii zao. 

Kufuatia mkutano huo mkuu, inatarajiwa kwamba viongozi wa kijadi na kidini wataendelea kuwa na jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu mara kwa mara kuhusu mpango wa Kuwabakiza Wasichana Shuleni barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Pages