MASHINDANO ya Taifa ya Wazi ya Mbio za Nyika ‘National Open
Cross Country 2019’ yanatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Gofu mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro, Februari 16 mwaka huu.
Kwa majibu wa Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, mashindano hayo yatakuwa maalum kuchagua timu ya
Taifa itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Nyika ya Dunia na
mwanariadha yeyote anaruhusiwa kushiriki.
Msimu wa 43 wa Mashindano ya Nyika ya Dunia unatarajiwa kufanyika
Aarhus, nchini Denmark, Machi 30 mwaka huu.
Zavalla, alisema mikoa yote imeishatà arifiwa rasmi kuhusu
mashindano hayo na wanariadha watakaofanya vizuri watachaguliwa timu ya Taifa.
Alisema mashindano hayo yatakuwa kwa upande wa Wanawake Sr,
Wanaume Sr, Wavulana Jr na Wasichana Jr.
Katibu huyo Msaidizi, aliongeza baada ya mashindano hayo ya
Taifa ya Nyika kumalizika, Kamati ya Ufundi itachagua makocha watakaoingia
kambini na timu itakayokuwa imechaguliwa mara moja huko Mbulu mkoani Manyara
kujiachia na mashindano hayo ya Dunia.
Mbio za Nyika za Dunia zilizopita zilifanyika barani Afrika, Kampala nchini
Uganda, 2017.
No comments:
Post a Comment