Na
Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali iliwalipa stahili
zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha baada ya
kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo ya madeni.
Hayo yamebainishwa Bungeni
Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Catherine Magige,
aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado
wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha
michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii wa PPF.
Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa
mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi zilikamilika na
wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni namba 46 ya mwaka 1931.
“Baadhi ya wafanyakazi
walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango
yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na
malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema Kiwanda hicho
kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na
PSRC mwaka 1995.
Aidha akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka
kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA
waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao.
Alisema Serikali
imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271 walistaafishwa na
madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao yao.
No comments:
Post a Comment