WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Bin Zubeir yaliyofanyika Kwamndolwa, Korogwe mkoani Tanga.
Akitoa
salam kwa niaba yake amesema “Rais Dkt. Magufuli aliweka nia ya dhati
kushiriki mazishi haya ila kwa bahati mbaya leo ana mkutano wa Wakuu wa
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha ambapo
yeye ni Mwenyekiti.”
“Mheshimiwa
Rais amenituma nije nikupe pole wewe, watoto, familia na wote
walioguswa na msiba huu. Mheshimiwa Rais anawaombea kwa Mungu ili mpate
utulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na nguzo katika
familia. Haya yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”
Waziri Mkuu ameshiriki mazishi hayo ya mke wa Mufti, Bibi Hidaya Omar leo (Alhamisi, Januari 31, 2019).
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewasihi wafiwa na waombolezaji wote waendelee kuwa
watulivu na kumuombea marehemu kila mmoja kwa imani yake ili Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.
Kwa upande wake,
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza
kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumtuma Waziri
Mkuu amuwakilishe katika mazishi hayo. Pia amewashukuru watu wote
waliojitokeza kwa ajili ya kuifariji familia kutokana na msiba
walioupata.
Viongozi
wengine waliohudhuria mazishi hayo niWaziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi
OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, Mhe. Salma Kikwete, Mhe. Hawa Ghasia,
Mhe. Mary Chatanda ,Mhe. Mkuu wa Mkoa wa TangaMartine Shigelana Masheikh wa Mikoa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,
ALHAMISI, JANUARI 31, 2019.
No comments:
Post a Comment