HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2019

UHONDO TAMASHA LA PASAKA WAREJEA DAR

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha la Pasaka litakalofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha la Pasaka litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waandishi wa habari.
 Waandishi wa habari wakiwa kazini.



NA MWANDISHI WETU

HATIMAYE uhondo wa Tamasha la Pasaka ambalo husindikizwa na kishindo cha muziki wa injili chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam, limerejea tena kivingine.

Tamasha hilo kongwe ambalo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2000, kwa miaka wili halikuweza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam kutokana na sababu maalumu zilizowahi kuelezwa na waratibu wa tukio hilo la kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Januari 21, 2019, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Ales Msama alisema baada ya tafakuri ya kina pia kwa kuzingatia maoni ya wadau wa muziki wa injili, wameamua kurejesha tukio hilo jijini humo.

“Kama mnavyojua, kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litatafanyika pia katika jiji hilo kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno,” alisema Msama.

Alisema mbali ya malengo ya msingi ya kueneza ujumbe wa Neno la Mangu na sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu, safari hii tamasha hilo litatumika pia kuhimiza hali ya amani chini ya kaulimbinu isemayo ‘Upendo, haki na Amani ndio msingi wa amani.’

Msama alisema kwamba, kwa kuzingatia uhalisia huo tamasha hilo litabeba agenda ya kuombea amani taifa na kumwombea Rais John Magufuli aweze kuongoza kwa ufanisi na mafanikio zaidi kwa maslahi ya watanzania wote.

Kwa upande wa maandalizi, Msama alisema tofauti na miaka mingi, safari hii wamejiandaa kuhakikisha linakuwa la kimataifa zaidi ikiwemo kuwaleta waimbaji mahiri wa kutoka nje watakaoshirikiana na wengine wa Tanzania.

Mbali ya Dar es Salaam, Msama alisema tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa mingine 10 ambayo itajulikana baadaye kwa kuzingatia vigezo stahiki vilivyowekwa na kamati ya maandalizi.

Chini ya maudhui ya msingi ya Tamasha hilo, ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia waimbaji, kukuza muziki wa injili ili kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya kuimba na kumiliki jukwaa na wauzaji wa kazi za kimuziki.

Tangu kuanza kwa tamasha hilo, waratibu wamekuwa walitumia sehemu ya mapato ya viingilio kuyafariji makundi maalumu katika jamii; walemavu, yatima pamoja na wajane.

Tukio hilo ndilo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kutokana na waratuibu kuwaleta waimbaji mbalimbali wa kimataifa kama Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope wa Afrika Kusini.

Waimbaji wengine ambao wamekuwa wakija kupamba tamasha hilo karibia kila linapofanyika, ni kutoka Kenya, Rwanda, DR Congo, Zamba pamoja na Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Pages