Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri
ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wakati wa kikao kazi
cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
Baadhi
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya
Wilaya ya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
(hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu Waziri
huyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani
Pwani.
Katibu
Tawala Mkoa wa Pwani, Bi. Theresia Mbando akitoa neno la utangulizi
kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na
watumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya
Kibaha, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao
chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
KIBAHA, PWANI
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) amempa onyo kali Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,
Bi. Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu
mstaafu aliyekuwa akidai haki yake na kumtaka afisa huyo ajirekebishe haraka
iwezekanavyo.
Onyo hilo
amelitoa wilayani Kibaha, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya
Mji wa Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika
wilaya hizo ili kujiridhisha na utekelezaji wake.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa
amesema, haiwezekani afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia Sheria, Kanuni na
Taratibu za kiutumishi ndio awe kikwazo cha utendaji kazi katika Halmashauri
hiyo kwa kutoa lugha chafu dhidi ya wanaofuta huduma ofisini kwake, na kuongeza
kuwa, afisa huyo ndiye anayestahili kuwa kwenye Kamati ya Maadili ili kutoa
miongozo ya uadilifu na kusimamia maadili ya watumishi kwa ujumla katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Mhe. Dkt.
Mwanjelwa amemtaka afisa huyo kutotumia cheo chake vibaya na badala yake
asimamie vema nidhamu na masilahi ya watumishi wa umma.
Sanjari na hilo,
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemtaka afisa huyo kuacha tabia ya kutoa siri za ofisi na
kutokuwa mchonganishi miongoni mwa watumishi wenzie kwani matendo hayo
hayapaswi kufanywa na mtumishi yeyote nchini.
Aidha, Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesema ameamua kuweka bayana mapungufu ya afisa huyo mbele ya watumishi
wenzie ili ajifunze kutokana na matendo yake yasiyoridhisha na aweze kubadili
mwenendo wake mbaya wa kimaadili.
Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameendelea kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma
nchini, kwa kutoa onyo kwa watumishi wote wanaobainika kukiuka
Kanuni za Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment