NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Mafuta ya Total, imepunguza bei ya mafuta yake kwa kutoa punguzo la Sh. 70,000 kwa kila lita ya mafuta, muda wa siku tatu, kuanzia Februari 13 hadi 15 katika baadhi ya vituo vyake katika baadhi ya mikoa,Tanzania nzima.
Kwa mujibu wa Meneja Operesheni Mtandao wa vituo vya Total, William Fillet, alisema uamuzi huo wa kupunguza bei ya mafuta katika vituo vya Total ni ili kuwapatia zawadi ya upendo wateja wao kwa lengo la kuwawezesha na wao kusambaza upendo kwa wengine, siku ya sikukuu hiyo ya Wapendanao ya Valentine kwa wateja wao, kwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea kwa pamoja.
Naye Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Total, Marsha Msuya Kileo, alisema sambamba na punguzo hilo la bei kwenye mafuta, pia wateja wote wa kike, watakaonunua chochote kwenye maduka ya Bonjur, yaliyoko kwenye kila kituo cha Total, watapatiwa zawadi ya maua ya Valentine kuonyesha upendo.
Marsha alisema, punguzo hilo, lenye kauli mbiu ya “Fill Up With Love”, yaani jaza mafuta kwa mapenzi. Marsha amewakumbusha Watanzania, kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha Total, haujazi mafuta tu, bali unajaza mafuta ya Total Excellium, ni mafuta yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo, kwa kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo, yakiboresha injini ya gari yako.
Jumla ya vituo 16 vya mafuta vya Total ndivyo vimeteuliwa kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.
No comments:
Post a Comment