NA KENNETH NGELESI,MBEYA
UMOJA wa wafanyabiashara wa Mbao Halmashauri ya jijni
la Mbeya wameunga mkono za Serikali katika changamoto ya ukosefu wa vyumba vya
madarasa katika shule ya Sekondari kwa kutoa msaada wa mbao 859 aina tofauti
tofauti zenye dhamani ya shilingi milioni 3.5 kwa ajili ya kupaulia vyumba vya
madarasa.
Akizungumza mara kukabidhi mbao hizo kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya James Kasusura, Mwenyekiti wawafanyabiashara wa
Mbao Jijini Mbeya,Mbasa Sanga alisema kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni kuitikia
wito wa Mkuu wa Mkoa Mbeya Albert Chalamila ambaye Jenuari 20 mwaka huu aliwandikia
barua ya kuwaomba msaaada wa mbao kwa ajili ya kupaulia vyumba vya madarasa.
Sanga alisema kuwa Mchango huo ni kuunga mkono
juhudi zilizo anzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye hivi karibuni aligawa
bati za kuezekea madarasa katika shule za Sekondari zilipo katika Wilaya
zilizipo Mkoa wa Mbeya.
Aidha Sanga aliongeza
kuwa wao kama wazazi na wanajamii wameona ni vema kuunga mkono juhudi zilizo
anzishwa na mkuu wa Mkoa kwa kutoa Mbao.
Alisema kuwa wamekubali ombi hilo na ndiyo maana
kuchangia mbao ili kuwawezesha watoto walioshindwa kuendelea na masomo licha ya
kuwa walifauli na waliapaswa kuwa madarasani tangu Jenuari walipo chaguliwa.
Sanga alisema kuwa baada ya kupokea barau hiyo waliwasiliana
na wanachama wao na walikubalia ombi la Mkuu wa Mkoa na kwamba licha ya kuwa
mbao hizo ni chache lakini wanaamini zitasaidia kupunguza tatizo na ukosefu wa
vyumba.
Alisema wao kama wadau wa elimu na wanambeya
wataendelea kujitolea kwa hali na mali na kwa nguvu zao zote kushiriki shughuli
zote maendeleo na hasa sekta ya elimu.
‘Tutajitolea kwa nguzu zetu zote ili kuboresha elimu
ya Jiji leti na Mkoa wetu kiuhalisi maendeleo ya Mbeya yataletwa na wanambeya
wenyewe hivyo niwaombe na wadau wengine watakao guswa wajitokeza kuunga mkono
juhudi na Mkuu wa Mkoa wetu’ alisema Sanga
Sanga alisema kuwa maendeleo hayana itikadi hivyo ni
wajibu wa kila mwana jamii katika Mkoa wa Mbeya kuona ni namna gani atashiriki
kutatua changamoto ya madarasa’
‘Maendeleo ni elimu na elimu ndiyo maendeleo na sisi
kama wazazi,hiili suala nisitazamwe kisiasa, wazazi tunaweza kuwa wanasaiasa
lakini watoto wanao soma katika shule hizi hawana vyama hivyo niwasii watu wote
tujitoe kwa hali na mali kuinua elimu yetu’ alisema Sanga
Akipokea Msaada huo kwa niadba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Mkurugenzi wa Halmashuri ya jiji la Mbeya James Kasusura aliwashukuru
wafanyabiashara hao kwa mchango huo kwamba mbao hizo zitakwenda kufanya kazi
iliyokudiwa na hakuna hata ubao mkoja ambao utapotea.
Alisema kuwa kitendo kilicho kilicho fanywa na
wafanyabisahra hao ni cha kizalendo na kipaswa kuungwa Mkono na wananchi wote
wa Jiji pamopja na Mkoa wa Ujumla kwani maendeleo ya Mkoa yataltewa na wanambe
wenyewe na wala wasitegemee mtu kutoka eneo linguine kuja kleta maendelo katika
mkoa wao.
‘Huu ni moyo wa kizalemndo ndugu zangu mbao hizi
zitafanya kazi kama ilivyokusudiwa lakini pia mnasema msaada huu ni kidogo sana
kiukweli ni mkubwa mbao hizi zitakwenda kupunguza changamoto hii vyumba vya
madarasa’ alisema Kasusura
...Siyo kwamba mbao zilikuwa hazina kazi, mngeweza kuuza
au kujengea nyumba zenu lakini kutokana moyo wenu wa uzalendo na upenda mlionao
kwqa watoto lakini pia kuwiwa na maendeleo ya wenu ndiyo maana mmetoa mbao
hizi’ alisema Kasusura
Akizungumza kwa naiaba ya madiwani watano ambazo
shule zitakazo nufaika na msaasa huo Diwani wa kata Ilomba Dickoson Mwakilasa (CHADEMA),alisema
kuwa wanaamini utakwenda kutatua changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa.
“Tunakwenda kutatua changamoto ya madarasa hivi sasa
tupo kwenye ujenzi na bati zilishatolewa na Mkuu wetu wa Mkoa lakini tulikuwa
hatuna mbao za kupauliawa hivyo tunakwenda kukamilisha madarasa na watoto ili
ifikapo mwishoni wa februali watoto waendelee na msomo”’ alisema Mwakilasa
No comments:
Post a Comment