NA JOHN MARWA
WAANDISHI wa Habari nchini wameombwa kuufahamisha uuma juu ya mchezo wa Karate ili kuondoa tafsiri tofauti zilizopo juu ya mchezo huo na kuufanya kupiga hatua, hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Karate nchini Tanzania Willy Rwezaula katika Semina ya Karate kwa Waaandishi wa Habari.
Semina hiyo iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam ilikuwa na lengo la kuwafahamisha na kuwaelimisha waandishi juu ya mchezo huo na jinsi gani ya kuripoti mchezo huo ili kuondoa ukakasi uliopo kwa jamii ili uweze kupiga hatua na kulitangaza taifa katika anga za kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika semina hiyo Rwezaula alisema mchezo huo uliingia nchini miaka ya 1970 hali inayoufanya kuwa mkongwe licha ya kuto piga hatua kama Taifa na kubaki kwa mtu mmoja mmoja kwani hadi sasa haujapewa kipaumbele licha ya kuwa ulijaliwa mwaka 2006.
Alisema lengo la kuandaa semina hiyo ni kutoa elimu kwa waandishi kwani wao ndo wenye dhamana ya kuuhabarisha umma juu ya mambo mabali mbali yanayoendelea katika jamii kwa kuamini kuwa kama tasnia ya habari itaupa kipaumbele kama inavyofanya kwenye michezo mingine basi utapiga hatua.
“semina hii ni maalumu kwa Waandishi wa Habari ili kutoa elimu ya mchezo huu, ili wanapo ripoti habari za karate basi wafanye hivyo huku wakijua ni nini hasa kilichomo ndani mchezo huu na watusaidie kueneza karate halisi kwa jamii, kuondoa sintofahamu zilizopo na kukuza mchezo huu hapa nchini,”alisema Rwezaula.
Awali akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji JKA/WF-Tanzania Nestory Fedeliko alisema Lengo la semina hiyo ilikuwa kutoa elimu kwa waandishi juu ya mchezo huo ili wanapoandika au kuripoti kwa namana yoyote ile habari zao ziwe katika muktadha unaostahili zaidi na kutoleta mkanganyiko katika Jamii ya Wachezaji wa Karate Nchini kwa kuzingatia aina na utofauti uliopo katika Mchezo huo.
“Baada ya kuona kwamba habari nyingi za karate haziripotiwi katika kiwango kinacho stahili na kutoa mkanganyiko kwa jamii ya Wanakarate, pia kutokana na upotoshaji na uzushi uliozagaa mitaani kwamba mchezo huu ni wa kihuni, haufai kuchezwa na kada fulani katika Jamii mfano Wanawake na sintofahamu nyingi zinazo fanana na hizo. Ndio maana sisi JKA/WF-Tanzania kwa kushirikiana na Tanzania Shotokan-Ryu Karate-Do Association (TASHOKA) tukaamua kwa pamoja kuandaa semina hii kwa Waandishi wa Habari ili kutoa elimu ya mchezo huu, ili wanapo ripoti habari za karate basi wafanye hivyo huku wakijua ni nini hasa kilichomo ndani mchezo huu na watusaidie kueneza karate halisi kwa jamii, kuondoa sintofahamu zilizopo na kukuza mchezo huu hapa nchini.
“Waandishi wa Habari kupitia vyombo vyao vya habari ndio nguzo muhimu ya usambazaji taarifa katika taifa lolote lile duniani. Hivyo tumeona tukiwaelimisha Wanahabari tutakuwa tumeelimisha idadi kubwa sana ya Watanzania na kwa kipindi kifupi. Pia kuwawezesha Waandishi kutambua mahali sahihi pa kwenda kupata taarifa sahihi za mchezo wa karate kama chanzo chao cha habari,”alisema Fedeliko na kuongeza kuwa.
Na si kama ilivyo sasa Wandishi wengi hawajui na hawatambui vyanzo maridhawa vya taarifa za karate. JKA/WF-TANZANIA na TASHOKA NI NANI?, Shirikisho la Japan Karate Association/World Federation - Tanzania (JKA/WF-Tanzania) ambao ndo waandaji rasmi wa semina hii kwa kushirikiana na Tanzania Shotokan-Ryu Karate-Do Association (TASHOKA), ni shirikisho la kimataifa la kijapani linalojihusisha na mchezo wa karate aina ya shotokan.
“Shirikisho hilo lilikuwepo hapa nchini tangu mwanzoni mwa mwaka 2006, ila lilipata usajili wake rasmi toka makao makuu Tokyo Japan mwaka 2007. Hadi sasa lina vilabu wanachama Zaidi ya 20 nchi nzima (Tanzania Bara na Visiwani). JKA/WF ndilo shirikisho Mama la mashirikisho mengi duniani yanayofanya shotokan karate. Na ndilo shirikisho kubwa la mchezo wa karate duniani mpaka sasa,”alisema.
Akieleza Mafanikio waliyoyapata hadi sasa alisema wamefanikiwa kuendesha semina na mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa, ndani na nje ya nchi, pia Kupunguza dhana ya upotoshaji juu ya mchezo halisi wa karate. Kwa kiwango kikubwa sasa wamewaelimisha watu na kuondoa dhana ya uhuni na si mchezo wa wanaume tu.
“Leo hii tuna wanawake wanaocheza karate, pia karate imeanza kutambuliwa mashuleni hadi serikalini kama mchezo rasmi unaofaa kufundishwa na kuliwakilisha Taifa letu katika nyaja na kimataifa, tumeweza kuwa na wanachama wenye viwango vya Kimataifa vinavyokubalika kote duniani: Madaraja ya mikanda (vyeo), ufundishaji (Instructor), uamuzi (Judge) na utahinishaji (Examiner), Kuhimiza uzalendo kwa nchi yetu. Pamoja na wanachama wetu kuwa na viwango na ubora wa kimataifa bado wameendelea kusalia nchini kulitumikia Taifa lao.
“Pamoja na mafanikio yote hayo, pia tuna changamoto kadhaa zinazotukabili, Vifaa Watu wengi wanashindwa kujiunga na huu mchezo ama kuishia njiani pale wanapokwama kutokana uhaba wa vifaa kama vile, Dojo (Ukumbi maalum ya kufanyia mazoezi) Mavazi rasmi, Vifaa vya kufanyia Mazoezi, Punching bags, mouth guards, gloves, head protectors, pamoja na Wafadhili (Sponsors).
“Tumekuwa na wakati mgumu sana kupata wafadhili, hasa pale tunapoandaa Semina, Mashindano na hata pale tunapotaka kupeleka timu yetu ya Taifa kwenda kushiriki mashindano ya Kimataifa nje, Kupewa nafasi ya kufundisha karate mashuleni Tuna walimu wengi wenye weledi mkubwa juu ya mchezo, na watoto tuliowafikia wameonesha kuukubali na kuupenda mchezo huu ila wanashindwa kujiunga sehemu zetu za mafunzo kutokana na gharama na umbali,”alisema.
Nae mwakilishi wa Mgeni Rasmi kutoka katika kampuni ya ‘SUKOS KOVA FOUNDATION’ ambaye ni Mratibu wa taasisi hiyo Mustapha Mkwama, aliwapomgeza kwa hatua waliyofikia na kuahidi kufikisha yale aliyoyasikia kwa Mkurugenzi wake Suleman Kova na kuona jinsi gani wataweza kuwasaidia.

No comments:
Post a Comment