HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2019

Airtel kutoa Tzs 2.1 bilioni kama faida kwa wateja wa Airtel Money

Meneja wa Huduma ya Airtel Money, FIDELIS KAIJAGE, akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitanga kugawa faida ya jumla ya Tsh 2.1 Bilioni kwa wateja na Mawakala wa Airtel Tanzania ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi sita iliyopita kati ya Aprili na Septemba,2018 . Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Airtel Jackson Mmbando, akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitanga kugawa faida kwa wateja na Mawakala wa Airtel Tanzania ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi sita iliyopita kati ya Aprili na Septemba,2018 . Kulia ni  Meneja wa Huduma ya Airtel Money FIDELIS KAIJAGE .


 
Dar es Salaam 14 Machi 2019:  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inatarajia kugawa faida ya jumla ya Tsh2.1 bilioni kwa wateja wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money

Faida itokanayo na  Airtel Money ni fedha ambazo Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia  Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kiwango hicho cha faida kwa kila salio la mteja kinatolewa pia kulingana na jinsi mteja anavyotumia huduma ya Airtel Money, mteja atatumiwa faida yake kwenye akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kuamua kuzitoa au kuzitumia kwa matumizi yoyote ikiwemo  kulipia bili mbalimbali kama vile za DAWASCO, LUKU na mengine mengi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kuanza kugawa  faida hiyo, Meneja wa Huduma ya Airtel Money FIDELIS KAIJAGE alisema “faida itokanayo na matumizi ya Airtel Money itagawiwa kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wote nchini ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi sita iliyopita kati ya Aprili na Septemba,2018 .

“Airtel inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali zanazochochea kusambaa na upatikanaji wa huduma za kifedha hapa nchini kwa kutoa faida kila robo ya mwaka, faida hii itawawezesha wateja kupata jumla ya Tzs2.1bn zitakazokwenda kwa wateja na mawakala waliotumia huduma kwa kipindi hicho. Tunayo furaha kuona ukuaji mzuri kwenye huduma ya Airtel Money kwani mpaka sasa huduma zetu zimekuwa zikikuwa mfululizo kwa ukuaji wa tarakimu mbili, alisema Kaijage.

Kaijage aliongeza kuwa hii ni mara ya saba Airtel inatoa faida kwa wateja wake wote wa Airtel Money tangu mwaka 2015. Mpaka sasa jumla ya kiasi cha Tsh 16 bilioni kimeweza kutolewa kama faida kwa wateja na mawakala wote nchini.

“Kuanzia leo wateja wote wa Airtel Money wataweza kutumia fedha zao za faida kwa kununua LUKU, kununua muda wa maongezi au bando au kwa matumizi yeyote yale”. Alisema Kaijage

Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta karibu huduma za Airtel Money ili kufikia maelfu ya Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki na hasa kwa maeneo ya vijijini. Kwa kufanikisha hilo, hivi karibuni Airtel ilizindua kampeni ya Tuko Nawe Kila Kona kwa lengo la kuimarisha huduma ya maduka ya Airtel Money Branches ambayo ni moja kati ya mikakati muhimu ya kusambaza huduma ya Airtel Money hapa nchini. Vilevile Airtel imezindua bando za Dabo Data Smatika kupitia Airtel Money kwa lengo la kuongeza huduma kwenye huduma zinazotolewa na Airtel Money branches zaidi ya 500 nchini

Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano Airtel JacksonMmbando alisema kuwa “Lengo letu ni kuendelea kuwafikia wateja wetu ambao ni muhimu sana kwenye biashara yetu. Tunatarajia kuzindua maduka ya Airtel Money Branches zaidi kwa miezi ya hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa na huduma za kifedha ambazo ni za hali ya juu zilizo panuka kuliko huduma yoyote ya kifedha nchini . Wateja wetu tunawahakikishia huduma ya papo kwa hapo za kutoa pesa ni BURE na vile vile ukiwa na Airtel Money bado utaweza kupata mikopo rahisi kutoka Airtel TIMIZA Mkopo ili kufanikisha jambo lolote la dharura,  vile vile ipo huduma ya kujiwekezea akiba kwa ajili ya matumizi ya baadae kupitia TIMIZA Vikoba.

Airtel Money inamawakala zaidi ya 60,000 nchini kote, Airtel bado itaendelea kuhakikisha ya kwamba inapanua wingo wa mawakala kwa ajili ya kufikisha huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa Watanzania wote mjini na vijinini.

Kulingana na utafiti wa TCRA wa hivi karibuni wa mwezi December 2018, inaonyesha kuwa huduma ya Airtel Money imekuwa kwa haraka na kufikia asilimia 25%. “Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa huduma ya Airtel Money pia tumejiunga na huduma zingine zenye tija kwa watumiaji kama vile e-government ambapo wateja wanaweza kufanya malipo ya huduma mbali mbali kwa wakati mmoja. Pia huduma ya Airtel Money imeunganisha zaidi ya benki 40 ili kuwawezesha wateja  kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu za mkononi kwenda benki na vile vile kutoa benki kuweka kwenye akaunti za simu za mkononi wakati wowote” alimalizia Kusema Mmbando.

No comments:

Post a Comment

Pages