Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto), akiwa katika Mkutano Mkuu wa
63 Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea katika jiji la New York
nchini Marekani.
Na Mwandishi Wetu – New York Marekani
Tanzania ni nchi mmojawapo duniani iliyofanikiwa
kupiga hatua katika kuwawezesha wanawake kijikwamua kiuchumi kwa kuwasaidia
kupata mikopo isiyo na riba inayowawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya
kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo na Mh Ummy Mwalimu, Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, katika Mkutano Mkuu wa 63
wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
unaoendelea New York, Marekani.
Waziri
Ummy alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua katika uwezeshaji wa wanawake
kiuchumi kwa kuwapatia fursa za mikopo na kufanyia marekebisho Sheria
ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018 ambayo imefuta Riba kwa
mikopo yote inayotolewa kwa wanawake kupitia Halmashauri.
Alisema
Halmashauri zimekuwa zikichangia asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kwa
ajili ya mikopo kwa wanawake, matokeo yake kiwango cha fedha
zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya mikopo ya wanawake kimeongezeka
kutoka bilioni 3.4 mwaka 2015/16 kufikia bilioni 16 mwaka 2017/18.
Waziri Ummy alieleza kuwa tangu mwaka 2015
Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kutoa elimu bure ya Msingi na Sekondari na
kufanya ongezeko la asilimia 80 katika uandikishaji wa watoto wa shule za
msingi na ongezoko la asilimia 20 kwa Sekondari.
Ameongeza
kuwa katika kuhakikisha
watoto wa kike wanapata elimu bila vikwazo vyovyote mwaka 2018 Serikali
imefuta
tozo ya kodi katika taulo za kike (pads) na hivyo kupelekea upatikanaji
wake
kuwa rahisi na kwa gharama nafuu ambapo mwanzo watoto wengi wa kike
walikuwa wanakosa vipindi madarasani kutokana na kukosa taulo hizo.
Katika huduma za afya, Tanzania imepiga hatua kubwa
katika utoaji wa huduma za afya hususan huduma za afya ya mama na mtoto pamoja
na maboresho ya miundombinu ya afya na chanjo. Kwa mwaka 2018/19 Kati ya vituo
vya afya 518, vituo 304 vimekarabatiwa ili kuboresha huduma za afya ya mama na
mtoto ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji na hivyo kuwa na jumla ya vituo 459
nchi nzima vinavyotoa huduma za dhalura na uzazi ukilinganisha na vituo 109
mwaka 2015.
Na
katika sekta ya nishati Waziri Ummy alieleza
kuwa Tanzania kupitia mradi wa umeme vijijini (REA) imeweza kusambaza
umeme
katika vijiji zaidi ya 7000 kati ya vijiji 15000 sawa na asilimia 46 ya
vijiji
vyote nchini hili limesaidia sana kuwawezesha wanawake kupata fursa
mablimbali kutokana na upatikanaji wa nishati hiyo kwa urahisi kuanzisha
miradi ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo vidogo.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Taarifa ya Utafiti wa Upatikanaji wa Nishati
Tanzania ya mwaka 2016 asilimia 32.8 ya kaya Tanzania bara zina Umeme, na asilimia
44.2 Zanzibar. Upatikanaji wa umeme umewezesha huduma za afya kupatikana kwa
wepesi hasa huduma za uzazi, upatikanaji wa maji na kurahisisha shughuli
zingine za uzalishaji mali kwa wanawake.
Mkutano wa
63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa wa Hali ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019
unaendelea jijini New York Nchini Marekani ukiwa na Kaulimbiu inayosema
"Mifumo ya Hifadhi ya Jamii, Huduma za Umma na Miundombinu Endelevu kwa
Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana".
No comments:
Post a Comment