Mabaki ya ndege iliyoanguka.
Mmoja wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo mbaya. Hapa ni mjini Addis Ababa, Ethiopia
Mwadada Hiba wa Djibout, akilia kwa kupoteza ndugu yake aliyekuwa akisubiri ndege hiyo namba 302 katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi Kenya.
Ndege iliyopata ajali.
Ndugu na jamaa waliopoteza uhai katika ajali ya ndege wakiwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole, mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ndugu za abiria waliokuwemo katika ndege iliyopata ajali wakiwa katika hali ya simanzi kuu katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, mjini Nairobi, Kenya.
ADDIS ABABA, ETHIOPIA
ABIRIA 149 na wafanyakazi wanane waliokuwa katika ndege ya
Shirika la Ethiopian Airlines iliyoanguka wanahofiwa kufariki dunia.
Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka jijini Addis Ababa kwenda jijini
Nairobi, ilianguka dakika sita tu baada ya kupaa katika Uwanja wa Kimataifa wa
Ndege wa Bole.
Akituma rambi rambi, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed,
amesema shughuli za uokoaji zinaendelea, na kwamba hawajabaini idadi ya
majeruhi wala waliofariki kufuatia ajali hiyo.
Amesema, shirika hilo litatangaza nambari ya dharura ambayo
jamaa na marafiki za waliokuwamo watatumia kuwasialiana kutafuta usaidizi.
Rais Uhuru Kenyatta ni kati ya viongozi ambao wametuma
rambirambi. Kupitia Mtandao wake wa Twitter Rais Kenyatta amesema amesikitishwa
na ajali hiyo.
Kupitia ukurasa wa twitter kwa waathiriwa wa ajali ya ndege
ya Ethiopia, amewapa pole familia na wote walioguswa na ajali hiyo.
Kiongozi wa ODM Raila Odinga amesema ni jambo la kusikitisha
kuwa watu wengi wamefariki dunia kufuatia ajali hiyo. Wengine ambao wametuma
rambirambi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mousa Faki.
Shirika hilo limesema litawatuma maafisa wake hadi katika
eneo la ajali ili kusaidia kwa njia zozote.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, abiria waliokuwamo ni
kutoka nchi 32 na wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat
Begashaw.
Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa
ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.
Taarifa rasmi ya Shirika hilo inasema walipoteza mawasiliano
na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege
wa Adi Ababa.
Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani
ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa,
aliliambia shirika la habari la kitaifa la Ethiopia msemaji wa Ethiopian
Airlines.
Kampuni hiyo inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa
kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Kwa upande wa idadi ya waliofariki, Kenya imepoteza watu 32,
Canada 18, Ethiopia (8), China 8, Marekani 8, Uingereza 7, Ufaransa 7; Misri 6
na Umoja wa Mataifa (UN) 4.
Wengine waliopoteza uhai na nchi zao ni India 4; Russia 3; Morocco 2; Israel 2;
Ubelgiji 1; Udanda 1; Yemen 1; Sudan 1; Togo 1; Msumbuji 1 na Norway 1.
No comments:
Post a Comment