HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 28, 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA KAZI YA UPAKAJI WA RANGI NDEGE YA FOKER 50 ILIYOKUWA IKITUMIWA KUBEBA VIONGOZI AMBAYO ITAANZA KUBEBA ABIRIA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama wakwanza (kushoto) pamoja na Richard Mayongela watatu kutoka (kushoto) ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kukagua kazi ya upakaji wa rangi katika ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali ambayo sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. (Picha na Ikulu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mafundi wazalendo ambao wamefanya kazi ya kuandika na kuchora nembo ya Twiga pamoja na kupaka rangi ndege hiyo ya Foker 50 kwa gharama ya  Shilingi milioni 7. Pia Rais Dkt. Magufuli amewazawadia mafundi hao kiasi cha Shilingi milioni 10 kutokana na kazi yao nzuri ya kizalendo walioifanya. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt. Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi miloni 7.
Rais John Magufuli akishuka katika ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba viongozi wa serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
 Sehemu ya Ndani na nje ya  Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo  awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora nembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.



No comments:

Post a Comment

Pages