Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars
katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika
iliyochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars
katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika
iliyochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars imeshinda 3-0 na kufuzu AFCON 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akishangilia baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza
mechi kati Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Machi 24, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda. Taifa Stars ilishinda 3-0. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezana na Rais wa TFF,
Wallace Karia baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mechi kati
Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini
Dar es Salam, Machi 24, 2019. Taifa Stars ilishinda 3-0. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa timu ya taifa ya Uganda. (Picha na Said Powa).
Simon Msuva akishangilia na John Bocco.
Simon Msuva akishangilia na John Bocco.
Furaha ya kupata goli.
YAMETIMIA TANZANIA YAFUZU MICHUANO YA AFCON
*Ni baada ya kuifunga Uganda the Craines magoli 3-0
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda 'The Crane' magoli matatu kwa sifuri.
Mechi
hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imechezwa katika Uwanja
wa Taifa leo (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.
Taifa
Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada
ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo
kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.
Magoli ya Simon Msuva, Erasto Nyoni na Agrey Morris yalichangia kuivusha Taifa Stars, ambapoMsuva
alianza kwa kuipatia gori timu ya Taifa ya Tanzania dakika ya 20 baada
ya mechi hiyo kuanza, Nyoni aliipatia Taifa Stars goli la pili dakika ya
50 na dakika sita baadae Moris aliipatia timu ya Taifa goli la tatu.
Kufuatia
ushindi huo wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania
wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10
kutoka kwaKamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza
na wachezaji hao jana wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao,
Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake
itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu
kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kwa upande wake,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala yeye aliwaahidi
kuwapeleka katika mbuga yoyote ya wanyama watakayoichagua kwa ajili ya
mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi dhidi ya
timu ya Taifa ya Uganda.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 24, 2019.
No comments:
Post a Comment