Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga. |
Kutokana na ukweli kwamba mazingira ya Uwekezaji yanakabiliwa
na dhoruba ambazo zaweza kuwa kubwa sana
au za wastani; saa nyingine dhoruba zikawa hazipo kabisa. Wewe kama mwekezaji
unayo kazi kuu moja ya kuhakikisha kuwa unaifikisha meli (Uwekezaji wako)
salama kule unapotaka ufike. Vinginevyo Uwekezaji kama meli unaweza ukishia
pasipo julikana baharini. Ili chombo kisizame shurti ujue unatoka wapi na
unakwenda wapi, na njia utakazo pita na changamoto zake uwe umezitafiti na
kuchukuwa tahadahari husika kabla ya safari, yaani wakati wa safari ukutane na
yale ambayo hata ungefanya vipi usinge juwa kama yatatokea.
Kwa hiyo basi kila kampuni ni lazima iwe na utaratibu wa
kukabiliana na athari zinazoweza kutokea katika Uwekezaji, kwa mfano katika
Uwekezaji wa pamoja meneja ni lazima awekeze katika maeneo mbali mbali, yaani
inapaswa akwepe kuweka katika kapu moja, hii ina maana ya kuwa kapu moja
likidondoka mengine yanakuwa yamesimama,
pia athari zinapunguzwa kwa kutumia utaalamu kwa maana ya kuwa ni lazima afanye
upembuzi wa kitaalamu kabla ya kuchaguwa ni wapi awekeze, kwa mfano kama
anakopesha uwezo wa aliyekopeshwa kulipa upo? Historia yake dhidi ya madeni
ukoje?; pia anaangalia mfumuko wa bei je kwa kuzingitatia utaalamu thamani ya
fedha inatarajiwa kuwa vipi?; anafanya tathimini ya hali ya uchumi na
siasa ya sasa na ya baadae ; na mambo
mengine kadha wa kadha.
Uwekezaji unaochukuwa
tahadhari dhidi ya dhoruba na majanga kabla ya kutokea na kuweka hatua zipi za
kuchukuwa kama hali hatarishi ikitokea.
Ukiwa ameangalia tahadhari zote kabla, utakuwa umejiweka vizuri katika
kutia wawekezaji imani kuwa hata wakati wa mawimbi mambo yatakuwa mazuri.
Tukichukuwa tahadhari kabla itasaidia katika maamuzi kwa mfano lipi lianze kwanza
na lipi lingojee, tuwekeze fedha zetu vipi? Na itatusaidia kutotoka sana njee
ya njia kuu ya kutufikisha katika mpango wetu huku tukitumia gharama ndogo
kukabiliana na tahadhari kama itatokea.
Sehemu muhimu za kuangalia mianya ya athari katika Uwekezaji ni kama kwenye
Sehemu muhimu za kuangalia mianya ya athari katika Uwekezaji ni kama kwenye
· Mpango mkakati-Kuingia kwa mshindani
sokoni
· Fedha-ongezeko la riba katika mikopo
· Matakwa ya Uwekezaji-kanuni mpya
katika Uwekezaji
· Utendaji-Uchovu au mitambo kuharibika
· Menejimenti- yaweza kuwa mbovu au
badilika
· Mazingira
· Uchumi
· Siasa n.k
Kama umechukuwa hatua kabla, janga likitokea unaweza libeba sababu gharama za kuliondoa ni kubwa sana, pia waweza kuhamisha tahadhari nah ii ni kwa kutumia bima, na wakati mwingine utapaswa kubadili mfumo mzima wa jinsi unafanya jambo Fulani. Cha muhimu uwe na sera juu ya majanga.
Kwa hiyo kiujumla tunaweza sema
kuwa tahadhari katika Uwekezaji wa pamoja ni kama zile za kwenye Uwekezaji
mwingine kwa mfano pesa za mfuko katika Uwekezaji zinakopeshwa kwa riba, riba
inapanda na kushuko kutokana na mwenendo wa soko la fedha. Riba ikishuka ina
maana faida kwa mkopeshaji inapungua.
Pia riba ikishuka thamani ya Uwekezaji inaweza pungua Pia mojawapo ya sehemu mifuko inawekeza ni kwenye kukopesha , ukikopesha aliyekopeshwa anaweza shindwa kulipa bahati nzuri UTT AMIS haikopeshi watu au taasisi binafsi, hukopesha serekali tu kupitia hati fungani , na mabenki kupitia akaunti za mda maalumu na pengine madeni kwa benki ya muda mfupi. Tahadhari nyingine ni Uwekezaji katika hisa, hisa zina tabia ya kupanda na kushuka, japo hisa ndiyo chachu ya faida wakati mwingine zinashuka na aidha kupunguza faida au kuleta hasara.
Pia riba ikishuka thamani ya Uwekezaji inaweza pungua Pia mojawapo ya sehemu mifuko inawekeza ni kwenye kukopesha , ukikopesha aliyekopeshwa anaweza shindwa kulipa bahati nzuri UTT AMIS haikopeshi watu au taasisi binafsi, hukopesha serekali tu kupitia hati fungani , na mabenki kupitia akaunti za mda maalumu na pengine madeni kwa benki ya muda mfupi. Tahadhari nyingine ni Uwekezaji katika hisa, hisa zina tabia ya kupanda na kushuka, japo hisa ndiyo chachu ya faida wakati mwingine zinashuka na aidha kupunguza faida au kuleta hasara.
Kumbuka
tukiongelea athari, mfano uchumi ukianguka haijalishi hela zako ziko wapi
lazima kwa namna moja au nyingine utaguswa. Lakini uzuri wa Uwekezaji wa pamoja
ni kwamba meneja (UTT AMIS) ana
wekeza sehemu nyingi hivyo basi kupunguza wastani wa mtikisiko wakati mambo
hayaendi sawa na pia kuongeza faida
wakati mambo yanakwenda vizuri.
Pia kabla ya kuendelea na Makala
tukumbuke kuwa meneja akiwekeza kwenye hisa, au ukawepo mfuko ambao unawekeza
kwenye masoko ya hisa tu, basi tunasema kuna nafasi kubwa ya kupata faida Zaidi
lakini pia tahadahri ni kubwa sana , na mara nyingi Uwekezaji wa sehemu hii
unahitaji muda mrefu.
Lakini meneja anayewekeza katika hati fungani na akaunti za muda maalumu anakuwa yuko salama Zaidi, hususani kwenye hati fungani za serekali. Kwa hivyo tunaweza sema dhoruba zina kwenda sambamba na pale tunapowekeza, ni kazi yetu kuhakikisha tunakabiliana na mawimbi makali na ya wastani sababu lazima yawepo na kuhakikisha chombo kinafika salama. Utaalamu wa hali juu na uzoefu pamoja na sifa nyingine ndo tiba.
Lakini meneja anayewekeza katika hati fungani na akaunti za muda maalumu anakuwa yuko salama Zaidi, hususani kwenye hati fungani za serekali. Kwa hivyo tunaweza sema dhoruba zina kwenda sambamba na pale tunapowekeza, ni kazi yetu kuhakikisha tunakabiliana na mawimbi makali na ya wastani sababu lazima yawepo na kuhakikisha chombo kinafika salama. Utaalamu wa hali juu na uzoefu pamoja na sifa nyingine ndo tiba.
Kwa kuwekeza katika sehemu
tofauti tunapata faida kwa kuwa hizi
sehemu tofauti zinakuwa na tabia tofauti pia. Kwa mfano mara nyingi hisa
zinapokuwa zinapanda basi riba kwenye hati fungani zinashuka. Hisa zinapokuwa
zinapanda wawekezaji wanakimbilia kuzinunua kwa kuwa wanajuwa watapata faida
lakini zinapokuwa zinakuwa kwenye mdororo wawekezaji wana kimbilia kwenye hati
fungani.
Cha kufanya ni nini?
· Tathimini
malengo yako ya kiuchumi/kifedha na kwa muda upi unafikiri utayafikia
· Tathimini
uthubutu wako katika Uwekezaji , utadhoofika kiasi gani kama faida au hata
mtaji utapungua
· Tathimini
gharama ziendanazo na Uwekezaji mzima
Epuka
- Kuchaguwa mfuko kwa sababu unafanya vizuri tu kwa sasa hivi. Yaweza kufanya hivyo kwa sababu tu ya faida muda mfupi. Anya utafiti kwanza pata historia ya mfuko na jaribu kuangali hali ya kibiashara ya sasa na baadae.
- Jaribu kupata ushauri kabla ya kuwekeza, tafuta wajuzi wa Uwekezaji wa namana hii kabla ya kuthubutu. Kwa kifupi njoo tuongee.
- Kumbuka bei ya kipande inaendana na mwendo wa soko, kipande kina weza pand au kikashuka. Hivyo basi thamani ya kipande ina panda na kushuka.
Cha muhimu ni kuwa kampuni ya
Uwekezaji ya UTT AMIS inasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana
(CMCA) , kazi kubwa ya Mamlaka ikiwa kuhakikisha kuwa taratibu za msingi za
Uwekezaji pamoja na mashart yake vinafuatwa ili kuepusha athari yeyeto ile kwa
Mwekezaji.
Pamoja na Mamlaka kuna wahasibu wa
serekali, kampuni binafis na wandani, pia kuna
Mwangalizi CRDB Bank, na Mkutano
Mkuu wa Wawekezaji kila mwaka vyote hivyi pamoja na utawala bora vikiwa ni
kuhakikisha kuwa Mwekezaji anapata haki zake kutokana na hali halisi na kama
ilivyo ainishwa katika Waraka wa Makubaliano.
Baada ya kuangalia tahadahri za Uwekezaji wa pamoja itakuwa
vyema kuangalia faida zake.
· Utaalamu,
ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuwa na utaalamu wa juu ya Uwekezaji kwenye
masoko ya hisa na mitaji, UTT AMIS kama mtaalamu anakusaidia hata kama
ungependa kuwekeza wewe kama wewe.
· Anuai, hata
kama ni kiasi kidogo cha fedha kitawekezwa sehemeu mbali mbali hivyo basi
kupunguza athari za Uwekezaji, mayayi yankuwa yameweka katika vikapu vingi.
· Mtaji, sio
lazima uwe na hela nyingi kama mtaji, kuanzia shilingi 10,000 tayari unakuwa
ndani ya Uwekezaji
· Uwazi,
unajuwa thamani ya mifuko na amana zako kila siku
· Ukwasi,
hakuna urasimu pale unahitajio sehemu au fedha zako zote
· Kodi,
unafuu wa kodi kwenye pato la mwisho
· Gharama,
gharama ndogo za uerndeshaji
· Muda,
unaendelea na shughuli zako zingine wakati meneja-UTT AMIS anasimamia Uwekezaji
wako.
Baada ya kufahamu faida na hasara,
anza kuwa mwekezaji. Kwanza kabisa weka lengo-kwanini uwekeze, halafu tengeneza
kanuni au taratibu itakayo kufikisha kwenye lengo lako. Chagua mfuko unaona una
kufaa. UTT AMIS ina mifuko 5, yaani Umoja, Watoto, Wekeza Maisha, Jikimu,
Ukwasi na pia ina huduma ya Usimamiziwa Mali (Wealth Management Service),
wekeza kwa muda mrefu unavyo weza ili kuipa faida jumusihi nafasi, na pia
kuweza kununua vipande katika bei tofauti tofauti, ukisha nunua vipande usiache
kuendelea kuongeza, nunua mara nyingi kadri unaweza.
Kumbuka bei ya kipande inaweza panda
au kushuka kutokana na mwendo wa soko.
No comments:
Post a Comment