Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dk. Anna Mghwira pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah wakipokea msaada wa mifuko 200 ya saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , inayotengeneza saruji ya Moshi
Cement , Tian Haifeng.
Sehemu ya mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Jun Yu inayoendeshwa na raia wa China iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari Polisi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dk. Anna Mghwira ,akiongizwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah kwa kutizama maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari zinazojengwa katika kambi ya Polisi Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dk. Anna Mghwira ,akizungumza jambo na Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah mara baada ya kutizama maendeleo ya
ujenzi wa nyumba za askari zinazojengwa katika kambi ya Polisi Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, akizungumza wakati wa kupokea msaada wa saruji kutoka kampuni ya Jun Yu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , Tian Haifeng akimwaga maji wakati Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira akinawa Mikono.
Dkt Mghwira akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , Tian Haifeng mara baada ya hafla fupi ya kupokea msaada wa Saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari Polisi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
FAMILIA 400 za askari
Polisi kati ya 1600 katika mkoa wa Kilimanjaro wanaishi uraiani hali
inayochangia kupungua kwa maadili katika utendaji kazi kwa baadhi ya askari kutokana
na kuishi maeneo yasiyokuwa kambi za Polisi.
Kutokana na hali hiyo tayari Jeshi la Polisi mkoa wa
Kilimanjaro limeanza ujenzi wa nyumba sita katika eneo la kambi za Polisi mjini
Moshi kwa ajili ya makazi ya askari hao baada ya kupokea kiasi cha Sh Milioni
150 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John Pombe
Magufuli.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji
kutoka kampuni ya kichina ya Jun Yu investment ,watengeneza wa saruji ya Moshi
Cement ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi
,Hamis Issah alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh Bilioni 10 zilizotolewa na
Rais.
“Nimshukuru mh. Raisi wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za dhati za kuboresha ustawi wa askari kwa kutoa shilingi Bilioni 10 kwa ajii ya kujenga nyumba za kuishi askari
polisi na familia zao katika mikoa yote nchini.”alisema kamanda Issah.
“Aidha siku ya leo kwa
niaba ya maofisa,wakaguzi na askari wa
jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro ,niushukuru
uongozi wa kampuni ya Moshi Cement kwa kutupatia mifuko 200 ya saruji na huu ni
mwanzo mzuri kwa wadau kuendelea kutusaidia.”alingeza Issah.
Kamanda Issah alisema uongozi wa kampuni ya Moshi Cement
wamejitoa kuchangia baada ya kufahamu umuhimu wa jeshi la polisi katika
shughuli zao za uwekezaji na pia katika
kumuunga mkono Mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ,Dkt Magufuli
katika juhudi za kuboresha jeshi la Polisi.
“Nyumba hizi zinatakiwa zikamilike ifikapo Juni 31 mwaka 2019
hivyo tunajitahidi kuwashirikisha wadau wa jeshi la polisi na wadau wengine wapenda maendeleo ili kukamilisha ujenzi huu kwa wakati,na pia
ikiwezekana tuongeze nyumba nyingine katika eneo hili .”alisema Kamanda Issah .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza
mara baada ua kupokea msaada huo alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha
askari wake wanaishi kwenye maeneo yaliyo safi na salama huku akieleza kuwa
shauku yake ilikuwa ni kuona ujenzi huo ni wa nyumba za Ghorofa.
“Nilipokuja kutembelea uwanja huu binafsi nilitamani sana
kama tungekuwa tumejipanga haya majengo yangeenda Juu ili kuacha nafasi ya
kutosha kwa ajili ya watoto wa askari na jumuiya inayoshi hapa ,kupata sehemu mbalimbali zikiwemo za mapumziko na biashara kidogo “alisema Dkt Mghwira.
Alisema ujenzi wa nyumba za Ghorofa zingetoa nafasi kwa
askari Polisi kuishi maisha ya Staha wanapokuwa kambini tofauti na ilivyo sasa
hali iliyowalazimu askari kuongeza vyumba katika nyumba wanazo ishi ili waweze
kuenea na familia zao.
“Nilitamani sana msingi huu ungetengenezwa kwa ajili
yakupanda juu lakini tukasema kwa sababu
serikali imetupa fursa hii ebu tuitumie hii kuwa kichocheo kwa ajili ya makazi
mengine yatakayo endelea yasibaki kuwa ya chini .” alisema Dkt Mghwira .
Kutokana na hali hiyo Dkt Mghwira alimuagiza Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah kukaa na waandisi kwa ajili ya kufanya
tathimini ya makazi yanayohitajika kwa ajili ya askari Polisi pamoja na gharama
za ujenzi wa nyumba hizo.
“ RPC kakae na wahandisi waturetee utaratibu wa kujenga
makazi yote yanayohitajika tukipandisha juu na tutahitaji fedha kiasi gani ,…tunaweza
kuanza kukusanya kidogo kidogo kama hivi
ninavyoona sasa,maana tunaweza
tukamaliza ujenzi hata kabla hatujaigusa ile pesa iliyotolewa na Rais Magufuli.”alisema
Dkt Mghwira .
“Na mimi kwa hili naomba niwahamasishe tena wana Kilimanjaro
,yeyote anaye jisikia kutenda lolote katika hili alete mchango wake kama sadaka
yake kwa ajili ya maisha na ustawi wa askari wetu ,kama mnavyoona eneo hili
liko wazi na linapakana na makazi ya watu na hakuna ukuta unaotenganisha maeneo
hayo , hili ni upungufu mkubwa sana ,”aliongeza Dkt Mghwira.
Tayari hadi sasa wadau mbalimbali wameendelea kutoa michango
yao ikiwemo kampuni ya Rocktronic iliyotoa Loli pamoja na Greda kwa ajili ya
kusafisha eneo la ujenzi ,Ravj aliyetoa kokoto tani saba , mfanyabiashara Mr
Ngowi aliyetoa mifuko 200 ya saruji pamoja na askari namba E 1708 Koplo Dickson
Mwakabuta ambaye ametoa mchanga Lori moja kwa hiari yake.
No comments:
Post a Comment