Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa, Tarimba Abbas, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana, kuhusu ujio wa timu ya Sevilla ya Hispania ambayo itacheza na kati ya timu za Simba au Yanga. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na Waziri wa
Utalii na Mali Asili nchini Tanzania Dk. Hamisi Kigwangala.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa
Utalii na Mali Asili nchini Tanzania Dk. Hamisi Kigwangala amesema kuwa ujio
wa klabu ya Sevilla ni fursa kubwa ya kuitangaza nchi kupitia vivutio vya mali
ya asili.
Kauli
hiyo, aliitoa juzi mara baada ya Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa
kutangaza kuwaleta Sevilla nchini kwa ajili ya ziara ya kimichezo.
Wakiwa
nchini, Sevilla ambao pia ni mabingwa mara moja wa La Liga, watacheza na moja
ya timu washirika wa SportPesa kati ya Simba au Yanga kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Kigwangala alisema kuwa ujio wa Sevilla nchini unatosha
kabisa duniani kuijua Tanzania kutokana na ukubwa wa klabu hiyo yenye mashabiki
wengi.
Kigwangala
alisema, hivi sasa watu wengi duniani watataka kuijua Tanzania na kuanza
kuonekana kwenye ramani ya dunia, hivyo ni fursa kwa nchi kutangaza utalii
uliojaliwa kupitia wachezaji hao.
Alisema
kuwa, serikali imepanga kuitumia fursa hiyo kwa kushirikiana na SportPesa kwa
lengo la kutangaza vivutio vya nchi kabla na baada ya mechi hiyo kuchezwa kati
ya Simba na Yanga.
“Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Utalii na Mali Asili hii ni fursa yetu
tunayotakiwa kuitumia vema kuitangaza nchi kupitia ziara ya Sevilla kuwaleta
nchini mabingwa hao mara tano wa michuano ya UEFA Europa ikiwa ni sehemu ya
maandalizi yao ya msimu mpya wa 2019/2020.
“Kwa
kupitia kwa Sevilla wenye wachezaji wakubwa wa kimataifa, kutasaidia kuitangaza
nchi watakapokwenda kutembelea vivutio vyetu vya asili tulivyojaaliwa hapa
nchini zikiwemo mbuga mbalimbali.
“Wachezaji
hao watakapokuwa kwenye hifadhi zetu misitu ya mbugani watapiga picha ambazo
watazisamba kwenye mitandao ambapo mashabiki watataka kuhoji ni wapi walipo na
kwanini wapo kwenye pori lenye wanyama pori baadaye na wao kuvutiwa na kuja
nchini.
“Kwa
kufanya hivyo, tutaongeza idadi ya watalii kuja nchini kutembelea na ninajua
wataka kwenda Zanzibar kutembelea huko, pia ni fursa nzuri ya kutangaza utalii
huko.
“Kwa kupitia ziara hiyo, tumetoa ofa kwa
Sevilla kwa kuwapeleka kwenye moja ya hifadhi zetu bure watakapofika hapa
nchini” Alimaliza Waziri Kigwangala.
SportPesa
ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na michezo na habari za burudani.
Kupitia majukwaa yetu tunatoa matokeo ya mechi papo hapo na kwa nchi nyingine
tunatoa huduma ya michezo ya kubashiri na ushindi kwa wateja wetu.
No comments:
Post a Comment