HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 15, 2019

Benki ya CRDB, UBA waongeza nguvu mradi wa Stiegler’s Gorge


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi dhamana ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza kabla ya kumakaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi dhamana ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge.
Kutoka kushoto ni Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dk. Bernard Kibesse, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere.

Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA), Usmani Isiaka.

Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakifurahia jambo.

 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani, akizungumza katika hafla hiyo.



Baadhi ya wawakilishi wa UBA.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. Hamis Mwinyimvua, akizungumza wakati wa hafla kukabidhi dhamana ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dk. Bernard Kibesse, wakati wa hafla hiyo.

Balozi wa Misri nchini, Mohammed Abulwafa, akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, akizungumza kabla ya kupokea dhamana ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwa na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dk. Bernard Kibesse, wakati wa hafla hiyo.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dk. Bernard Kibesse, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.

Kubadilishana mawazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA), Usmani Isiaka akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, dhamana ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na Balozi wa Misri nchini, Mohammed Abulwafa (katikati).



NA FRANCIS DANDE

BENKI ya CRDB ikishirikiana na Benki ya UBA Tanzania zimeweka dhamana ya Dola milioni 737.5 za Marekani kwa ajili ya mradi mkubwa wa umeme wa Stigler's Gorge unaofanyika wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani.

Mradi huo wa umeme unatekelezwa na Kampuni ya Elsewedy Electric ya Misri kwa Sh. Trilioni 6.6 huku ukitarajiwa kuzalisha megawati 2,100 zitakazoingizwa kwenye gridi ya taifa na kurahisisha upatikanaji wa nishati hiyo kwa gharama nafuu.

Akikabidhi mkataba wa makubaliano ya kuweka dhamana hizo za kibenki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Ally Laay kwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Tito Mwinuka walisema lengo ni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana hapa nchini.

Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema dhamana hiyo ilitakiwa na mkandarasi wa kiarabu huku akibainisha kwamba mradi huo ni mkakati wa serikali tangu miaka ya 1960.

“Sisi CRDB tumeamua na tupo tayari kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais Magufuli kwa vitendo, huu ni ushirikiano wenye kulenga kuifikia Tanzania ya viwanda kwa umeme wa uhakika na gharama nafuu.

“Tumeshiriki kwenye miradi mingine ukiwemo wa REA lakini huu ni mkubwa… tunaposema Tanzania ya viwanda bila umeme wa uhakika haitakuja ndio maana tumeshirikiana na wenzetu UBA kuhakikisha dhamira hii ya serikali inakamilika,” alisema Nsekela.

Baadhi ya viongozi walioshuhudia makabidhiano hayo ni Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohammed Abulwafa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. Hamis Mwinyimvua, Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Dk. Bernard Kibesse.

No comments:

Post a Comment

Pages