HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2019

Hatimaye Mariam mwenye kidonda kikubwa mgongoni awasili Muhimbili


Na John Stephen, MNH

Mariam Rajab (25), mkazi wa  kitongji cha Inung'una,mkoani Singida, mwenye kidonda mgongoni, ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, hatimaye amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), saa sita usiku wa Jumatano, April 17,2019.

Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura, ambapo anaendelea kufanyiwa vipimo vya awali na kisha atalazwa, ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu zaidi siku ya alhamisi.

Msemaji hospitali ya taifa Muhimbili Bw.Aminiel Algaesha aliuatangazia umma juzi kwamba matibabu ya mgonjwa huyo  yangegharimiwa na hospitali hiyo.

 “Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu.Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni” hayo ni maelezo aliyotoa Mariam kupitia picha ya video iliyoanza kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii.

Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB) aliuagiza uongozi wa MNH kumtafuta Mariam popote alipo ili apelekwe hospitalini hapo kwa ajili uchunguzi na matibabu.

Mariam ameletwa Muhimbili kwa gari la wagonjwa almaarufu ambulensi kutoka mkoani Singida, lililoanza safari yake saa 8:00 mchana jana.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi juu ya mwenendo na maendeleo wa matibabu ya mgonjwa huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages