NA MWANDISHI
WETU
MKUU Wa Mkoa Wa Dar Es
Salaam, amesema kasi inayoendelea katika ujenzi wa Ofisi ya Waalimu Shule ya
Sekondari Kisauke iliyopo Wilaya ya Kinondoni Kata ya Wazo hili.
Amesema lengo la
ujenzi Wa Ofisi hiyo ya waalimu ni Kuona Waalimu wanaishi katika mazingira
mazuri na matumaini yake mwisho Wa mwezi Wa 5 Ofisi hiyo itakuwa
imekamilika.
"Tumeona tujenge
Ofisi hii kwanza kuwapa heshima Waalimu kwani wanavyotumia choo kimoja na
Wanafunzi inashusha heshima na inapelekea baadhi ya wanafunzi kupewa kesi za
utovu Wa nidhamu hivyo kukamilika huku tunategemea tunakwenda kutengeneza
Mazingira rafiki kwa Waalimu wakiwa katika Mazingira mazuri hata matokeo
yatapatikana mazuri kwani watakuwa na uwezo Wa kubuni mikakati ya kufaulu kwa
wanafunzi" anasema Makonda.
Aidha Makonda
aliongeza na kusema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo ni kukagua miradi ya
Maendeleo ili kile kilichopo kwenye karatasi kiendane uhalisia, ipo
miradi mbali mbali inayotekelezwa ikiwamo miradi ya ujenzi wa Hospitali, vituo
vya Afya na Masoko .
No comments:
Post a Comment