Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali Bungeni leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi
na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019. Mwingine pichani ni Naibu Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (Mb).
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
inayo dhamira ya kukamilisha skimu zote za umwagiliaji ambazo utekelezaji wake
haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo
tarehe 15 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Azza Hillal
Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la
Umwagiliaji katika Kijiji cha Ishololo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mhe
Mgumba amesema kuwa Skimu hiyo ipo miongoni mwa skimu za umwagiliaji zitakazopewa
kipaumbele katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (Irrigation
Master Plan 2018 - 2025) ambao kwa sasa umeanza kutekelezwa.
Alisema
kwa kuzingatia umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo mradi wa umwagiliaji Ishololo, tayari
Serikali imekwishaanza mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Japan
kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kwa lengo la kuboresha miradi yote
ambayo haijakamilika na ile inayofanya kazi chini ya ufanisi uliokusudiwa.
Naibu
Waziri huyo wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) alisema kuwa mradi wa ujenzi wa
bwawa wa Ishololo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini ni
moja kati ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji katika
Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika.
Alisema
Utekelezaji wa Mradi huo ulifikia ukomo wake mwezi Desemba 2013 ambapo Benki Maendeleo
ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji
wake ukiwa haujakamilika.
No comments:
Post a Comment