HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 15, 2019

UTUMISHI YAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, akifurahia jambo na wasaidizi wake baada ya ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. (Picha na Ofisi ya Rais-Utumishi).


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeanza kutoa huduma katika ofisi zake kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa huduma katika Mji wa Serikali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema, ofisi yake iko tayari na imejipanga kikamilifu kutoa huduma kwa wananchi na wadau wote wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa wananchi, watumishi wa umma na wadau wengine kufuata huduma katika ofisi yake iliyopo Mtumba kwenye Mji wa Serikali na kuongeza kuwa, kwa sasa Idara zilizohamia ni ya Utawala na Utumishi wa Umma na ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu ambazo zina wateja wengi, hivyo watumishi wa umma na wananchi wajitokeze kupata huduma.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, mwananchi au mtumishi yeyote mwenye uhitaji wa kupata huduma kutoka kwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wafike katika ofisi za Mtumba ili waweze kuhudumiwa ipasavyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Aprili, 2019, alizindua rasmi ofisi za wizara zilizojengwa katika Mji wa Serikali na kuelekeza Watumishi waanze kutoa huduma kwa wananchi mapema iwezekanavyo.


IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
 TAREHE 15 APRILI, 2019

No comments:

Post a Comment

Pages