Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji
wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi katika mechi ya ufunguzi wa Michuano
ya AFCON U17 ambapo Tanzania ilipambana na Nigeria kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, Aprili 14, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Shirikisho ya Soka Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad katika mechi ya ufunguzi ya Mashindano ya AFCON U17 kati ya Tanzania na Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Aprili 14, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiikagua Timu ya Tanzania ya Serengeti Boys iliyopamba na Nigeria katika mechi ya Ufunguzi wa Michuano ya AFCON U17 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Aprili 17, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mashindano ya AFCON U17 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam Aprili 14, 2019. Wenye Jezi za Bluu ni Timu ya Tanzania – Serengeti Boys na kulia ni Timu ya Nigeria.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua
mashindano ya AFCON U17 na kutangaza kuwa kuanzia kesho Watanzania wataingia
bila kulipia.
Ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumapili, Aprili
14, 2019) kwenye ufunguzi wa michuano hiyo iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye
ufunguzi wa michuano hiyo, aliambatana na Rais wa Shirikisho la Soka na barani
Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kukagua timu zilizofungua dimba na kisha akatangaza
uamuzi huo wa Serikali.
Timu zilizofungua dimba leo ni Serengeti Boys
ya Tanzania na Nigeria. Katika mchezo wa leo Nigeria imeibuka kidedea
baada ya kuifunga Tanzania mabao 5-4. Hadi mapumziko timu ya Nigeria ilikuwa
ikiongoza kwa mabao 3-1.
Mabao ya Nigeria yalipatikana dakika ya 20, 29,
36, 71 na 78 wakati mabao ya Tanzania yalipatikana dakika ya 21, 51, 56 na 60
ambapo magoli mawili kati ya hayo, yalipatikana kwa njia ya penati.
Bao la kwanza la Tanzania lililofungwa na
Alphonce Mabula Msanga lilitinga kimiani dakika ya 21. Bao la pili,
lilipatikana dakika ya sita ya kipindi cha pili na lilifungwa na Kelvin Pius
John.
Dakika tano baadaye, Morice Michael Abraham aliipatia
Tanzania bao la tatu lililofungwa kwa njia ya penati. Kabla vijana wa Nigeria
hawajakaa sawa, dakika nne nyingine, Edmund Godfrey John alitinga kimiani bao
la nne, ambalo pia lililifungwa kwa penati.
Timu ya Tanzania iko kundi A na imepangwa na
timu za Nigeria, Uganda na Angola. Michuano hii inatarajiwa kumalizika Aprili
28. Endapo timu hiyo ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys itaibuka na ushindi
katika michezo yake miwili, itakuwa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya
dunia kwa vijana wa umri wa miaka 17 yatakayofanyika mwakani huko Brazil.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, APRILI 14, 2019.
No comments:
Post a Comment