Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Dkt. Bashiru Ally,
akieleza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, wakati wa mashindano ya
kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Mtoto Summayya Juma, akionesha uwezo wake wa kuhifadhi Qur'an katika mashindano yaliyofanyika Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shaaban (kushoto) na baadhi ya wadau wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akimkabidhi zawadi Mtoto Summayya Juma, aliyeshiriki mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdalah Kijaji (katikati) na baadhi ya viongozi wa Dini Wilayani Kondoa wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, wakizungumza jambo wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa dodoma Mustapher Shaaban, akieleza umuhimu wa elimu ya Dini katika kuleta umoja wa kitaifa, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akimpongeza Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(kulia), kwa jitihada za kuhamasisha elimu Jimboni kwake, wakati wa mashindano
ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pahi Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma
wakishuhudia mashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wanamashindano ya kuhifadhi Qur'an Wilayani Kondoa
Mkoani Dodoma wakisikiliza wito wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt.
Bashiru Ally (hayupo pichani), kuhusu kuwa wabunifu katika Nyanja ya Sayansi na
teknolojia ili kuisaidia jamii inayowazunguka.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dk. Bashiru Ally, amewataka watanzania
kutumia uwezo wa kuhifadhi Vitabu
vitakatifu kuongeza ubunifu katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia na nyingine
ili kuendeleza jamii kwa kuipatia maendeleo stahiki.
Dk.
Bashiru ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani
Dodoma, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha wadau
kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Alisema
kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwekeza kwenye elimu kwa watoto, kwa kuwa
watoto wakisoma si tu wanajengewa maarifa lakini pia wanaunganishwa na hivyo
kuwa chachu ya kuweza kuisaidia jamii inayowazunguka.
Mratibu
na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dk. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la
mashindano hayo ya kuibua vipaji vya watoto vya kusoma Kitabu Kitukufu cha
Qur'an na kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na ujasili katika kueleza wanayo
yaamini yakiwemo mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali.
Kwa
upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia
Ackson, alisema kuwa kazi zinazofanywa na Dkt. Ashatu Kijaji, ni zakupigiwa
mfano hasa kwa wanawake na akawataka wazazi katika Wilaya ya Kondoa kumuunga
mkono kwa kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuinua elimu katika eneo hilo,
kwa kuhakikisha wanawapeleka watoto katika makambi yaliyo na lengo la kuongeza
ufaulu wa wanafunzi.
Mgeni
Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Mustapher Shabaan, amewapongeza vijana
walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi Qur'an na
kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa
kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na
kupata thawabu kutoka kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment