HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2019

Hakuna mpaka tena katika mawasiliano

.Yaja na kampeni ya Mpango Mzima
  
Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma mpya na ‘Kijanja’ itakayomwezesha mtumiaji wa mtandao huo kutumia intaneti yenye kasi  na ukubwa  wa (GB 5) bila kikomo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mawasiliano iitwayo 'Mpango Mzima'
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akionyesha namna ya kujiunga na huduma mpya ya Halotel iitwayo 'Mpango Mzima'



NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Halotel Tanzania imekuja na huduma mpya ya mawasiliano iitwayo ‘MPANGO MZIMA’ ambayo mbali ya faida nyingine, inamwezesha mtumiaji wa mtandao wa Halotel kupata unafuu wa huduma mbalimbali za simu.

Kuanzishwa kwa huduma ya Mpango Mzima ni muendelezo wa kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Halotel katika kumrahisishia mteja wake kupata huduma bora za mawasiliano zikiwemo za kutumia Intaneti bila kikomo, kupiga simu matandao yote bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms). 

Akiziungumza  kuhusu  ‘Mpango Mzima’ Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son alisema ujio wa huduma hiyo mpya  na ‘Kijanja’ imelenga kumwezesha mtumiaji wa mtandao huo kutumia intaneti yenye kasi  na ukubwa  wa (GB 5) bila kikomo.
Pamoja na Intaneti hiyo mtumiaji wa mtandao huo pia ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote bure kwa kila dakika 5 za kwanza na kupewa sms 5000 atakazozitumia katika kipindi cha mwezi mzima.

“Huu ni muendelezo wa mpango wa mapinduzi ya kimawasiliano wa Halotel kuwa karibu na kuwajali wateja wetu kwa huduma bora. Kuanzishwa kwa Mpango Mzima kutamwezesha mteja wetu wa Halotel kutumia intaneti ya kasi kubwa , kupiga simu bila kikomo kwa mitandao yote bure kila dakika 5 za mwanzo na hivyo kumuondolea hofu ya simu kukatika kabla hajamaliza maongezi” amesema Son.

Amesema ili mteja aweze kufaidika na huduma hiyo mpya anapaswa kujiunga  kwa kupiga *148*66# na kuchagua Mpango Mzima ambapo  ataweza kujiunga na kuwa  tayari kwa kuanza kufurahia unafuu huo mahususi kwa ajili ya watumiaji wa mtandao  wa Halotel.

Nguyen Van Son amesema huduma ya Mpango Mzima ni mpya kuwahi kutolewa na mtandao mwingine wowote wa simu hapa nchini na kuwaambia watumiaji wa Halotel kuwa hiyo ni zawadi kwao hivyo wanapaswa kuifurahia na kuitumia wakati wote.

Alisema Halotel pia imeweza kuunganisha Optic Fiber zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 20,000 katika maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa data kwa maeneo mapya na hivyo kuiwezesha kuwa chaguo la kwanza kwa wateja pale linapokuja suala la huduma za Internet.

No comments:

Post a Comment

Pages