Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Nyamkongo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma Wakishusha mabati kutoka kwenye gari la Benki ya NMB muda mfupi kabla ya NMB Bank kukabidhi msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule na Meza na Viti 126 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB – Margaret Ikongo, akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Chiwe na Meza na Viti 126 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za Wilayani Kongwa. Msaada huo una thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika shule ya Nyamkongo.
Spika wa Bunge Job Ndugai akikata utepe kama ishara ya kupokea msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Chiwe na Meza na Viti 126 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za Wilayani Kongwa. Msaada huo una thamani ya shilingi Milioni 10. Wengine katika Picha ni Mjumbe wa Bodi ya NMB – Margaret Ikongo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa – Zuberi White (Kulia Kwake) na Kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji, Bidhaa na Matumizi ya Digitali wa NMB - Pete Novat na Meneja wa NMB Kanda ya Kati Nsolo Mloz.
Spika wa Bunge Job Ndugai akimshukuru Mjumbe wa Bodi ya NMB – Margaret Ikongo mara baada ya kupokea msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Chiwe na Meza na Viti 126 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za Wilayani Kongwa. Msaada huo una thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yalifanyika leo shuleni Nyamkongo.
Spika wa Bunge Job Ndugai akimshukuru Afisa Mkuu Uendeshaji, Bidhaa na Matumizi ya Digitali wa NMB - Pete Novat mara baada ya kupokea msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Chiwe na Meza na Viti 126 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za Wilayani Kongwa. Msaada huo una thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yalifanyika leo shuleni Nyamkongo.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Nyamkongo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wabeba viti na meza muda mfupi baada ya NMB kuwakabidhi msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule na Meza na Viti 126 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yalifanyika leo shuleni hapo.
Spika wa Bunge - Job Ndugai akimshukuru Meneja wa Kanda ya NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi mara baada ya kupokea msaada wa Mabati 250 kwaajili ya ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Chiwe na Meza na Viti 126 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za Wilayani Kongwa. Katikati ni Afisa Mkuu Uendeshaji, Bidhaa na Matumizi ya Digitali wa NMB - Pete Novat. Msaada huo una thamani ya shilingi Milioni 10. Makabidhiano hayo yaliyofanyika shuleni Nyamkongo.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameiomba Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi ili wajue jinsi ya kutunza fedha za mikopo yao.
Ndugai ameyasema hayo wakati benki hiyo ikikabidhi viti 63 na meza 63 kwa Shule ya Mnyakongo pamoja na mabati 250 kwa Shule ya Chiwe zilizopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika amesema kuwa NMB wanakila sababu ya kuendelea kutoa elimu ya utunzaji fedha kwa wananchi kama wanavyofanya kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili wawe na ujuzi zaidi. Aidha amesema kuwa watu wengi wanakopa fedha lakini hawajui wafanyie nini baada ya kuzichukua. "
Yaani unashangaa muda mchache ukikutana na watu hao hakuna cha maana walichofanyia badala yake wanarudi katika maisha yya chini badala ya kusonga mbele kimaisha’’amesema Ndugai Spika Ndugai amesema kutokana na hilo kuna sababu ya elimu hiyo kutolewa kwa wananchi ili wakope fedha huku wakijua wanakwenda kuzifanyia nini.
Ndugai amefafanua kuwa ameshakutana na kesi hizo nyingi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wamekopa bila ya kupata mafanikio yoyote.
"Kwa kweli kwa hilo naomba mlifanyie kazi kwani limekuwa likiwaumiza wananchi na kupelekea kurudi nyumba kimaendeleo badala ya kwenda mbele katika maisha kupitia fedha walizokopa’’ amesisitiza Ndugai Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi amesema kuwa wataendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivyo wametenga maeneo manne kwa ajili ya kusaidia jamii.
Mlozi ameyataja amaeneo hayo ni Elimu,Afya,Kilimo na utunzaji Fedha kwa vijana mpaka watu wa rika la juu kwa lengo la kuwainua kiuchumi kwa kunufaika kwa kupitia NMB.
Hata hivyo amesema kuwa mpaka sasa tayari milioni 400 zimeshatolewa kwa ajili ya misaada katika shule na hospitli ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mlozi amesema kuwa NMB iko pamoja na serikali kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea. Naye Mkuu wa Shule ya Mnyakonga Mpokeeni Sanga amesema kuwa walikua na upungufu wa madawati 70 na wanaishukuru NMB kuwapa viti 63 na meza 63 na ambavyo wanaamini vitasaidia kupunguza uhaba waliokuwa nao.
Sanga amewahakikishia NMB kuwa vitu hivyo watavitunza ili hapo wanafunzi wengine waje kuvitumia hapo mbeleni na amewaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii kwani wamekuwa mfano wa kuigwa nchini.
Mkuu wa shule ya Chiwe Aron Mango amesema kuwa mabati hayo waliopewa yatawasaidia kuezeka mabweni ya wasichana ambayo yanajengwa shuleni hapo
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania - Job Ndugai ameishauri Benki ya NMB kuanzisha mpango wa elimu ya ujasiliamari na utunzaji fedha mashuleni ili kuwaandaa wanafunzi kujiajiri mara wamalizapo masomo.
Mh Ndugai aliyasema hayo leo wilayani Kongwa wakati wa halfla ya kupokea msaada wa Mabati 250 kwaajili ya shule ya sekondari chiwe na viti 63 na meza 63 kwaajili ya shule ya sekondari Nyamkongo zote za wilayani humo.
Ndugai alisema kuwa watanzania wengi wanakosa elimu ya ujasiliamali hivyo akaishauri Benki ya NMB kujikita kwenye kutoa elimu hiyo mashuleni ili kuwaandaa wanafunzi kuweza kujiajiri pindi wamalizapo masomo na kuongeza idadi ya watanzania wenye nidhamu ya matumizi ya fedha kwa maendeleo yao.
“Benki ya NMB Mkipata siku chache zxa kufundisha wanafunzi mashuleni nchini kote kwa sababu nyinyi mpo kila mahali, elimu hiyo itawasaidia vijana wetu watakao ajiliwa na kujiajiri,” alisema Ndugai.
Aidha Ndugai alisema kuwa watu wengi wanakopa hela benki lakini hawajui wafanyie nini baada ya kuzichukua. Hivyo elimu ya fedha inahitajika kwa makundi yote.
Ndugai aliongeza kuwa “Nimeshakutana na kesi kutoka kwa marafiki zangu, wanakopa lakini ukiwauliza baada ya miezi kadhaa fedha mmefanyia nini, wanasema hawajui imeenda wapi na hawajafanya cha maana chochote, hivyo elimu mtakayo itoa itawasaidia.”
Alisema hiyo inawaumiza sana wananchi na kupelekea kurudi nyuma badaala ya kwenda mbele katika maisha kupitia fedha walizokopa.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi alisemaa NMB inatenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kila mwaka kwaajili ya kusaidia jamii kupitia afya, elimu na majanga mbalimbali.
“NMB tumeamua kushirikiana na shule hizi (Mnyakongo na Chiwe ) bila kusahau jamii yote inayozunguka shule hiii kwa kuchangia mabati na madawati kwa ajili ya shule ya sekondari (Mnyakongo na Chiwe ) vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ujumla” alisema Bwana Nsolo
“Mpaka sasa tayari tumeshatoa Zaidi ya shilingi milioni 400 kwaajili ya kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali nchini.” Alisema
Nsolo aliongeza kuwa Katika eneo la elimu Benki ya NMB imekuwa ikitoa madawati kwa shule za msingi, viti na meza kwaajili ya shule za sekondari na vifaa vya ujenzi kwaajili ya ujenzi ya miundombinu ya shule.
Alitaja eneo la Afya ambapo Benki imetoa msaada wa vifaa tiba, mashuka, vitanda vya kawaida na kujifungulia na unjenzi wa miundombili ya hospitali mbalimbali.
Nae Mkuu wa shule ya Nyamkongo - Mpokeeni Sanga aliwashukuru Benki ya NMB kwa msaada walioipatia shule na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo kwa manufaa ya muda mrefu Zaidi.
Huku Mkuu wa shule ya sekondari Chiwe - Aron Mango alisema mabati waliopewa yatasaidia kuezeka maabara ambayo itasaidia wanafunzi kujifunza na kumudu masomo ya sayansi.

No comments:
Post a Comment