Mgeni
rasmi Tullo Chambo akisalimiana na wachezaji wa Ibdhu FCwakati wa
ufunguzi wa Ligi ya Swaiba Cup 2019 kwenye uwanja wa Ngunguti Vikindu
Mkuranga mkoani Pwani. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mratibu wa mashindano hayo, Asha Mbata, alisema akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.
NA MWANDISHI WETU, MKURANGA
TIMU
ya Ibdhu FC imeanza vyema katika michuano ya Swaiba Cup, baada ya juzi
kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Zamalek FC, katika mchezo wa
ufunguzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Ngunguti, Vikindu Wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani.
Huo ni msimu wa pili wa michuano
hiyo ya Swaiba , ambayo yanalengo la kukuza vipaji vya vijana na
kuwaondoa katika makundi yasiyofaa.
Katika
mechi hiyo ya ufunguzi, mabao ya Ibdhu FC yalifungwa Ibrahim Karumbi
aliyepiga 'hat trick' na Babu Funga, huku ya Zamalek yakifungwa na
Selemani Doweko na Ally Adebayor.
Mratibu wa mashindano hayo, Asha Mbata, alisema michuano
hiyo imeandaliwa na kampuni Ibdhu Company Ltd, lengo ni kujitangaza
kibiashara na biashara zake ambazo zipo Iringa Mafinga, Vikindu Mkuranga
Pwani, Dar es Saalam na Sumbawanga.
"Lakini
pia ni kuunga mkono sera ya serikali ya kukuza vipaji, pamoja na
kuwaweka vijana pamoja ili kuwaepusha na makundi yasiyofaa," alisema.
Alisema mashindano hayo yamegawanyika katika makundi manne ya timu tatu, huku washindi wawili watakwenda hatua ya robo fainali.
Mbata,
alisema mshindi wa kwanza atapata Ng'ombe na mpira mmoja, wakati wa
pili Mbuzi na mpira mmoja, huku watatu ni mpira mmoja.
Ligi hiyo iliendelea jana kwa mechi moja kati ya Toyo FC vs Ibdhu Academy.
No comments:
Post a Comment