Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali
Alfred Kapinga ( Kushoto ) akiagana na
Kamanda Kikosi Kundi la 13 Luteni kanali Khalfan Kayage (Kulia )
kinachoenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan leo mei 16 wakati wakiondoka
kwa Ndege ya ATCL (Haipo pichani ) katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es
Salaam katikati ni Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi. (Picha na
Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali
Alfred Kapinga Akiagana na Maafisa na
Askari wa JWTZ Kundi
la 13 linalokwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan wakati
wakiondoka kwa Ndege ya ATCL (haipo Pichani) leo Mei 16 katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa JWTZ Kundi la 13 wakijiandaa kuondoka kwa Ndege ya ATCL leo Mei 16 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es
Salaam kwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan.
Na Luteni Selemani Semunyu
Maafisa na Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza
kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa
Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono
jitihada za Mhe Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi
kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na
Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi
inayoongozwa na Uzalendo, uadilifu, uhodari hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshi na wapiganaji kuunga mkono jitihada za
Serikali katika Kuboresha Uchumi ikiwa
ni sehemu ya mchango wao katika kuonesha
uzalendo kwa vitendo kwa kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana
ya Taifa.
“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa
tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini
sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege
zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.
Aidha, Meja Jenerali kapinga alisema mbali
na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha
wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus
Matindi Alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL
na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa
majeshi ya Ulinzi kwa Mchango mkubwa kufanikisha
kupata tenda hiyo.
“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa
Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza
na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa
maslahi ya Nchi “ Alisema Mhandisi
Matindi.
Vilevile Mhandisi
Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12
bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa
tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya
kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.
Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13, Luteni Kanali Khalfan Kayage anayekwenda na
Kikosi hicho alisema kuwa inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia
Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya
Tanzania Kimataifa.
No comments:
Post a Comment